Home Kitaifa Tigo na StarTimes wanakuletea kombe la dunia kiganjani mwako

Tigo na StarTimes wanakuletea kombe la dunia kiganjani mwako

9328
0
SHARE
Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Tigo, William Mpinga (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa kampeni ya Tukio Kubwa Zaidi la Soka Duniani.

Mashabiki wa soka nchi nzima wana sababu ya kushangilia kufuatia ushirikiano mkubwa kati ya Tigo Tanzania na StarTimes utakaowezesha Watanzania kutazama ‘laivu’ kwenye simu zao za mkononi mechi zote za tukio kubwa zaidi la mpira wa miggu kwa mwaka 2018.

Huku joto la msimu mkubwa zaidi wa soka kwa mwaka 2018 likizidi kupanda, kampuni inayoongoza kwa maisha ya kidigitali ya Tigo Tanzania imetambulisha tovuti ya michezo ya www.tigosports.co.tz itakayokuwa hewani kuanzia tarehe 14 Juni mwaka huu.

 

Meneja wa Masoko na Matangazo wa StarTimes, David Malisa akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa kampeni ya Tukio Kubwa Zaidi la Soka Duniani.

Tigo pia imeungana na mrushaji rasmi wa Kombe la Dunia, StarTimes kuzindua StarTimes Application, itakayowezesha wapenzi wote wa soka kuwa sehemu ya msisimko, furaha na huzuni yanayoendana na tukio hilo linalotazamwa zaidi duniani.

‘Tigo sports portal www.tigosports.co.tz itawezesha watanzania kufurahia msisimko wa dakika zote tukio kubwa zaidi la soka duniani kupitia mtandao mpana zaidi wa Tigo 4G, pamoja na kupata habari za matukio na dondoo muhimu za tukio hilo kubwa zaidi la mpira wa miguu duniani.

Afisa wa Habari wa StarTimes, Sam Gisayi akionesha hatu aza kujiunga na huduma mpya ya StarTimes App itakayowezesha wapenzi wa soka kutazama mechi zote 64 za kombe la Dunia laivu kwenye simu zao za mkononi.

Kwa kujiunga kupitia huduma iliyoboreshwa ya *147*00#, wateja wetu pia wanaweza kushiriki katika shindano litakalowapa nafasi ya kushinda zawadi za hadi TSH 10 milioni,’ alisema William Mpinga, Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa  Tigo.

Tigo inajivunia kwa mara ya kwanza kabisa, kuwaletea mashabiki wa soka  maajabu ya tukio hili kubwa zaidi la soka moja kwa moja kwenye simu zao za mkononi. Hii inaendana na sifa kuu ya Tigo ya kuwaelewa wateja wake na kuwapa bidhaa na huduma bunifu zinazoboresha maisha yao ya kidigitali.

Kwa kupakua StarTimes Application inayopatikana kupitia Applestore au Play Store, Watanzania sasa wanaweza kuchagua bando za saa, siku, wiki au mwezi kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*00#. Kisha wataweza kutazama mechi zote 64 za tukio kubwa zaidi la soka duniani kwa mwaka 2018 moja kwa moja kwenye simu zao janja wakiwa popote nchini huku wakifurahia ubora wa hali ya juu wa huduma za intaneti za Tigo 4G, mtandao mpana, wenye kasi ya juu na wa uhakika zaidi nchini.

‘Teknologia yetu ya StarTimes App inawezesha wateja wetu kuokoa gharama kubwa za intaneti, hivyo kuwasaidia kufurahia Kombe la Dunia muda wowote na popote walipo. Hii ni muhimu hasa ukizingatia kuwa baadhi ya mechi zinaanza saa 11 jioni, muda ambapo wengi wetu bado tupo ofisini au njiani kuelekea majumbani. Kwa hiyo Startimes App na Tigo intaneti zitahakikisha kuwa hukosi mechi yoyote,’ Meneja wa Masoko na Matangazo wa StarTimes, David Malisa alibainisha.

‘Mtandao wetu mkubwa  zaidi wa Tigo 4G unaopatikana katika miji 22 nchini, pamoja na uzinduzi wa sports portal na ushirikiano huu na Startimes ambayo ni kampuni kubwa ya kidigitali nchini, tutahakikisha kuwa hakuna shabiki anayepata kisingizio cha kukosa kutazama mechi laivu, kujua matokeo na kufuatilia dondoo mbalimblai za tukio hili kubwa zaidi la soka duniani kwa mwaka 2018,’ William Mpinga, Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Tigo alimalizia.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here