Home Kimataifa #RoadToRussia, Nike wajitoa kuivalisha Iran viatu dakika za majeruhi

#RoadToRussia, Nike wajitoa kuivalisha Iran viatu dakika za majeruhi

8859
0
SHARE

Macho na masikio ya kila mpenda soka kwa sasa yameelekezwa nchini Urusi ambapo katila siku tatu zijazo michuano mikubwa ya soka duniani ya kombe la dunia inaanza kupigwa katika viwanja tofauti nchini humo.

Moja ya mataifa washiriki ni Iran ambao wanaamini msimu huu wa kombe la dunia ndio msimu ambao watafanya vizuri kutokana na kujiandaa vyema, lakini sasa timu ya taifa ya Iran imekumbwa na tatizo.

Kampuni ya vifaa vya michezo ya Nike ambayo ndio ilitegemewa kutoa viatu kwa wachezaji wa Iran katika michuano hiyo imejitoa, sababu kubwa ya Nike kujitoa katika suala hilo ni vikwazo vya kiuchumi ambavyo Marekani wameweka kwa baadhi ya mataifa ya Asia.

Inasemekana taarifa ya Nike kujitoa imeichanganya kambi ya timu ya taifa ya Iran kwani imekuja katika wakati ambao muda umekwenda na sasa inabidi kutafuta namna ya kufanikisha suala hili.

Katika taarifa ambayo Nike wamewaandikia Iran inasema “vikwazo vya kiuchumi kwa baadhi yenu inamaanisha sisi kama kampuni ya Marekani hatutaweza kutoa viatu kwa timu yenu katika wakati huu”

Shirika la soka nchini Iran limetuma barua kwa FIFA kuwaomba mwongozo wao kuhusu suala hili, huku kocha msaidizi wa zamani wa Manchester United ambaye ni kocha mkuuwa Iran Carlos Queiroz akilitaja hili kama janga.

“Wachezaji wetu wamekuwa wakipewa huduma hii na Nike na mwaka 2014 walivaa vitu vyao, sio sahihi kwa Nike kufanya hivi katika kipindi hiki” alisema Queiroz. Inasemekana baadhi ya wachezaji wa Iran imewabidi kuazima viatu kwa wachezaji wengine wasioenda Urusi na wengine wakinunua madukani.

Serikali ya Marekani imeiwekea nchi ya Iran vikwazo vya kiuchumi kutoka na mzozo wa silaha za kinyuklia ambapo Marekani na kampuni zake hawawezi kuisaidia katika nyanja yeyote kiuchumi kwa sasa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here