Home World Cup Mats Hammels amemdharau sana Leroy Sane

Mats Hammels amemdharau sana Leroy Sane

11927
0
SHARE
Leroy Sane ameachwa. Maswali mengi yamejaa akilini mwa wapenzi wengi wa Soka. Hili suala limekuja na sura tofauti. Ballack amesema sio fea kabisa. Kyle Walker amemdharau sana kocha wa ujerumani kwa kufanya maamuzi mabovu. Draxler mwenyewe ameumia sana.

Yajayo yanafurahisha. Binafsi mimi sikupendezwa na maamuzi ya Jog Low. Amefanya maamuzi kama anataka kukosoa watu. Amefanya maamuzi ya kimalaika kwenye kundi la wanadamu. Unapomuita Mchezaji unamjengea Uzoefu unampa majukumu na heshima kubwa mabegani mwake.

Hakuna dhambi kubwa kama kudharau uwezo wa mtu kwa kuangalia zaidi hisia zako.

Mats Hammels nimemdharau mara 10 ya nilivyomdharau Jog low. Hammels ametoa kauli za kitoto sana ambazo binafsi namuona mnafiki tu. Sijui niseme amekaa kishamba shamba. Yaani anataka kuonesha kwamba yeye aliyechaguliwa ni bora kuliko yule aliyeachwa. Amemuona Thomas Muller Kama Lionel Messi watano.

Ameikwaza jamii ya vijana wadogo wanaochipukia ambao wana lengo la kuwakilisha mataifa yao. Unaropoka vipi wakati kama huu? Huo ushauri wake wa kinafiki alikuwa wapi siku zote. Amedhamiria kuonesha ubaguzi wa kijinga. Namuona kama hajakua kisoka. Hili ni fundisho hata kwa manahodha na wachezaji wetu wa bongo.

Mats amesema eti Sane asijione bora kabisa kwa Ujerumani. Yaani yeye sio levo za akina Mueller na Ozil. Kwani nani alisema Sane ni mchezaji mkubwa?

Sasa najiuliza 2014 aliyewapa kombe Ujerumani si alikuwa kijana mdogo? Amesahau Brazil 2002 ilikuwa na takribani nusu ya wachezaji ambao hawakuwa na majina?

Kuna tofauti kubwa ya Klasi ya mchezaji na Fom ya mchezaji. Kuna tofauti kubwa sana kati ya mchezaji ambaye ni mzoefu na mchezaji mwenye kiwango bora kwa wakati huo. Kinachomweka mtu uwanjani sio uzoefu tu bali kiwango chako pia. Ndiyo Maana leo hii Defoe na Lennon wapo nje ya kombe la dunia lakini Lingard na Rashford wameenda.

Mats anasema eti anakerwa sana na tabia za vijana wadogo wa Kijerumani wanaolalama kwenye mitandao. Sasa masikini kijana wa watu Sane wala hajongea chochote chenye ubaya kwemye mitandao. Sane hajafanya presi yeyote kulalamilia kutokuitwa kwake.

Kwanza anaposema kwamba Sane ni mchezaji mchanga hivyo kuachwa kwake ni sawa naona hakumbuki Sakata la Thomas Muller huyo huyo ambaye ameona Sane asifananishwe nae. Kwanza hakuna mchezaji anayeshushwa. Hata Messi hakushuka akawa star kesho yake akabeba Ballon d’Or.

Kwanza tutapima vipi uwezo wa Sane timu ya taifa kama hajitumi kwa michezo 12 ambayo kati yao ni michezo minne tu kacheza dakika 90? Hivi majuzi Mario Gotze si aliachwa kikosi cha awali? Kwanini Mats hakutoa huo ushauri wake kwa vijana? Kwanini amesubiria Sane atemwe ndipo ajikute mshauri? Hiyo kazi ya ushauri kaanza lini? Kazi ya ushauri yeye kama nahodha wa zamani kama aliona kuna kitu hakipo sawa kwa Sane kwanini asingemfuata binafsi na kumweleza?

Nimeangalia kwa namna Sane alivyobeba huzuni hii kama mwanaume. Kwanza ameandika kwenye ukurasa wake kushukuru wote wanaompa moyo. Amesema amekubaliana na maamuzi ya mwalimu na anaamini wakati ujao atarudi vyema na anaitakia Ujerumani kila la heri. Sasa huyu aliyekuja na maneno yake ya shombo anawafundisha nini wachezaji wetu wa ndani kama sio ushubwada?

Nina amini leo hii Samatta akiulizwa kwanini Ndemla ameachwa haweza kutoa kauli mbovu kama za Mats.

Mats ana matongotongo anahitaji wa kumfuta. Amesahau Kuwa Muller aliitwa timu ya taifa akiwa hajawahi kuichezea timu ya taifa michezo hata 10 kabla ya kuitwa timu ya taifa. Muller aliitwa na Jog Low kwenye kikosi cha timu taifa akiwa ameicheze Buyern munichen michezo 38 tu.

Sane kaanza kuitwa timu ya taifa 2015-2018 na kucheza mechi za kirafiki kadhaa. Sane mpaka sasa ametimiza michezo 86 ya ushindani wakati Muller alicheza michezo 38 tu na akajitwalia nafasi.

Sane ana uzoefu wa miaka 5 kwa mechi za mashindano. Sasa huo uchanga wa ushindani ambao umefanya adharaulike hadi na Mats ni upi?

Tena niwajibu tu wale ambao wanaoona kama Sane kutokufunga mechi kadhaa hizi za kirafiki. Mwaka 2016 Muller alicheza michezo 13 bila kufunga bao lolote tena akiwa kama mshambuliaji tegemezi. Sane huyu ni winga je kweli kipimo chake ni hizo mechi 13 za kimataifa tena za kirafiki?

“Leroy Sane sio mchezaji wa muhimu kwenye timu, hawezi kuthaminika kama Thomas Muller au Mesut Ozil,” Hummels ndo ameongea haya maneno. Siriazi?

Yaani amesahau kuwa Muller licha ya kwamba hakuwa na michezo mingi na hakuwa na uzoefu lakini alipoitwa kule Afrika kusini alifanya maajabu? Muller si ndo alibeba kiatu cha dhahabu kule Afrika kusini?

Hivi wanaamini kuwa Sane hajui umuhimu wake kwenye timu? Bahati kila mtu amezaliwa nayo wala hakuna mtu anampangia mtu bahati yake. Mario Gotze alikuwa amekalia bao lake benchi alipoingia alikamlisha biashara ambayo Muller na Close walishindwa.

Sane huenda angepambana zaidi ya hata tunavyomuona. Huwezi kupima kombe la dunia na vijimechi uchwara za kirafiki.

KAULI ZA MATS HUMMELS HIZI HAPA.

Mats akasema tena “wakati fulani inachukua mchezaji kufanya vyema kwenye timu ya taifa. Unapaswa ujitume ujitoe na upambane kwa hali na mali”

Hapo ni kweli wala sipingani nae lakini narudia tena Mario Gotze hakuwa na uzoefu wowote timu ya taifa. Kufunga goli wala hakuhitaji uzoefu wowote kunahitaji uwezo tu. Sipingani na uzoefu lakini tusikremu maisha. Kila mtu ana siku zake na nafasi njema mabzo anaweza kutumia vyema.

akaendelea kusema
“Hawa vijana wa siku hizi wana maisha yao. Ni vijana na wana mambo mengi. Wakiachwa wanalalamika. Kuwa mchezaji wa taifa hakuji hivi hivi”

Kwanini amesubiri kipindi Sane ana huzuni na kuongea pumba zake? Dunia nzima ya wapenda soka inamfariji sana, anatokea mlima mpunga mmoja anakwenda na kumsema Sane vibaya utadhani ameua? Kwani huyo Brandt aliyeitwa au Timo Warner wana umri wa vile vibabu vya Filamu ya Harry Porter au? Mbona kuna vijana wamepewa nafasi licha ya kwamba wana Umri mdogo? Kwanini hilo suala la Mambo mengi la vijana wadogo alione baada ya Sane pekee yake? Huyu Hammels ana shida gani kwani?

Akaendelea kusema.
“Nilikuwa kijana mdogo hapo awali, nilikuwa najituma ili kutimiza malengo, hilo ni jambo la kawaida. Siku hizi unakuta vijana wadogo hawajielewi, hawajitumi yaani wapo wapo tu. nawashangaaga sana”

Sasa huyu jamaa sijaelewa hapo anataka kusema Sane hajitumi au? Yaani kuna mtu mtu wa kudharau mbungi la Sane msimu huu? Kwanza kuna mtu angeamini kwamba Sane angekiwasha hivyo msimu? ndugu zangu mimi naona huyu jamaa anazeeka vibaya.

Akajaribu kuongea hisia zake

“Nilipojiunga Buyern nilikuwa siongei na mtu hata mmoja. Nilikuwa naongea na akina Stephan Furstner na Michael Rensing maana ndio nilokuwa nawajua kwenye chumba cha kubadilishia nguo. watu wengine nilikuwa nawasalimia tu To ‘hello’, au nawakaushia. Lakini siku hizi vijana hawa wadogo wakijiunga tu kwenye timu wanakuwa vimbelmbele utadhani wameichezea hiyo klabu miaka mitatu”

Kwani huyu jamaa ana matatizo gani, ndo maana nimesema huyu jamaa sio mzima. Ina maana mchezaji mdogo kuzoeana kwa haraka na wachezaji wakubwa kwake yeye anaona nongwa? Huyu jamaa hayupo sawa. Niaminini mimi kuna mawali aidha stresi za mahusiano au ana ushamba kama wa warombo wa Mamsera. au lazima kuna shida iliwshi kutokea vyumba vya kubadilishia nguo ambapo Sane aidha alimkera sio bure.

Mats ni mropokaji tunaweza kusema. Hajui kuishi kama mchezaji mkubwa. Yeye alipaswa kuwa mtu wa kwanza kumtia moyo Sane. Mats amezaliwa maisha ya soka. Alikulia Buyern wakati baba yake akiwa kocha wa timu ya vijana. Mama yake ni Mwandishi wa habari za michezo. Sasa sielewi kwanini amtolee Sane maneno kama haya kwamba eti yeye sio mchezaji wa muhimu sana.

Au tuseme kwakuwa Sane mweusi kwahiyo haoni umuhimu wake? la hasha tusifike huko.

Mats ni mtu ambaye huwa hawezi kujizuia kuongea. Ukurasa wa LB Life blogger unasema Mats hajui kuzuia kuongea kitu ambacho kitaumiza wengine. Na huenda hii ndiyo sababu kubwa iliyomnyima maisha ya Furaha Borussia. Akiwa Borussia yeye alikuwa nahodha. Lakini mbeba majukumu mengi kama kufanya mahojiano na kuongea na vijana wadogo kwenye timu ilikuwa kazi ya Sebastian Kelh. Mashabiki wengi walilalamika kuwa Mats haongei sana. Kumbe jamaa aligundulika hana kauli hivyo alipigwa marufuku.

Makala hii imeandaliwa na Privaldinho (Instagram)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here