Home Kitaifa Shaffih Dauda kuhusu Mo Simba Awards 2018

Shaffih Dauda kuhusu Mo Simba Awards 2018

17474
0
SHARE

Shaffih Dauda amepongeza tuzo maalum ambazo zimeanzishwa na mwekezaji wa Simba Mohammed Dewji zitakazojulikana kama Mo Simba Awards.

Tuzo hizo zitakuwa zikitolewa kwa wachezaji viongozi na mashabiki wa timu hiyo.

“Mo ni mfanya biashara anajihusisha na Simba kwa ajiki ya ku-push bidhaa zake kitu ambacho hakifanyiki kwa kificho wala sio dhambi, hiyo ni faida kwake kuwa mwekezaji wa klabu.”

“Anavyokuja watu hawatakiwi kuangalia kama Mohamed Dewji mpezi wa Simba, Mo ni brand na amewekeza kwenye tuzo. Ni jambo jema ambalo halijawahi kufanyika kabla na litaleta changamoto miongoni mwa wachezaji wa kikosi cha Simba.”

“Washindi wa tuzo zitakazotolewa katika vipengele mbalimbali watakuwa na deni kuhakikisha msimu ujao wanaendelea kufanya vizuri abaki kwenye tuzo.”

“Kwa wengine watajiuliza kwa nini huyu ashinde tuzo kutoka idara ya kiungo wakati na mimi nipo? Ataongeza jitihada ili na yeye ashinde tuzo.”

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya Mohammed Dewji inasema tuzo hizo zitafanyika kwa mara ya kwanza June 11, 2018  zikiwa na vipengele 16.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here