Home Kitaifa Babu wa Keko kaanza mipango kuwania tuzo Ndondo Cup 2018

Babu wa Keko kaanza mipango kuwania tuzo Ndondo Cup 2018

9761
0
SHARE

Shabiki wa Keko Furniture Abdul Pius maarufu kama Babu wa Keko ameshaanza maandalizi mapemaaa kuhakikisha anakamata tuzo ya shabiki bora wa Ndondo Cup msimu huu.

Babu wa Keko anakwambia tayari ameshaanza mazoezi kabla hata hatua ya makundi (32 bora) haijaanza kisa tu anataka kulamba tuzo ambayo amekuwa akiikosa kwa misimu kadhaa.

“Mwaka huu kitu cha kwanza nilichojifunza ni kwamba, huwezi kufanya jambo lolote ukafanikiwa bila kufanya mazoezi kwa hiyo mimi na crew yangu tunafanya mazoezi.”

“Ndondo Cup imenisaidia sasa hivi nimekuwa msanii na kuna vitu vyangu vingi navifanya kwa hiyo watu wasubiri. Nimeshafanya kazi kuhusu Ndondo ya msimu huu nimeelezea kisanii maana ya #Wastuewana.”

“Mwaka huuzawadi ya shabiki borabwa Ndondo Cup inanihusu.”

Keko Furniture ipo Kundi A pamoja na Boom FC, Makongo Sec na Mabibo Market. Game ya ufunguzi itaikutanisha Keko Ferniture dhidi ya Mabibo Market siku ya Ijumaa Juni 8, 2018.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here