Home Kitaifa “Tulibeza mipango ya Manji”-Sanga

“Tulibeza mipango ya Manji”-Sanga

12694
0
SHARE

Kaimu mwenyekiti wa Yanga Bw. Frank Sanga ameweka wazi baadhi ya mipango ya aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuf Manji lakini mipango hiyo ilipigwa chini na wanachama na kuonekana haifai.

Sanga ameeleza pia namna Manji alivyoingia kwenye uongozi wa Yanga na malengo yake matokeo yake aliishia kujiuzulu baada ya kuona mipango yake haiendi sawa.

“Manji aliingia Yanga kama mtu aliyekuja kutatua migogoro ambayo ilikuwepo kwa muda mrefu, alituunganisha tukawa kitu kimoja.”

“Hatua ya pili alihisi hajaona mafanikio akiwa nje kama mfadhili wa kawaida, akaona ni vyema awe kiongozi, alipokuwa kiongozi ndiyo tukaingia pamoja.”

“Moja ya mkakati mkubwa ilikuwa ni kuona na kuendesha lakini kulikuwa na changamoto za uendeshaji uongozi kupitia kamati ya utendaji ya watu ambao wamechaguliwa kwa aina ya watu ambao wanaingia pale kwa utashi wa Yanga.”

“Baada ya kuingia kama mwenyekiti wa Yanga na mimi makamu, tulikuwa na kamati ya utendaji kwa ujumla tunafanya kazi pamoja lakini kulikuwa na changamoto zake ambazo nyingine sio za kuzizungumza.”

“Akaona kuna njia nyingine ya kwenda kwenye mabadiliko ya katiba ya kufanya mwenyekiti na makamu kuwa kwenye kapu moja na wao kuunda kamati ya utendaji, mabadiliko hayo yaliridhiwa na mkutano mkuu ambapo tulipelekea kuunda kamati ya utendaji ya kuteua ambayo nadhani ndiyo kamati ya utendaji iliyofanya kazi vizuri katika kipindi chote.”

“Tulikuwa na mfumo sahihi wa mawasiliano lakini pia tulikuwa na watu ambao tuliwahitaji kwa ajili ya maendeleo ya Yanga lakini pamoja na hayo tulipomaliza kipindi chetu cha miaka miwili ndani ya miaka minne tulilazimika kufanya uchaguzi. Maelekezo yakatoka TFF na BMT kwamba tufuate katiba ya zamani kwa sababu mabadiliko hayakuwa yamesajiliwa.”

“Tukakubaliana kutofanya uchaguzi ule, lakini tukakutana na changamoto zilezile tulizokutana nazo mwanzoni nadhani ndiyo maana mwenyekiti alikuja na njia nyingine ya kuendesha timu kwa njia kuikodisha.”

“Yalikuwa ni mawazo yake ya kutaka kuikodi timu, alikuwa tayari kutoa shilingi 100M kila mwaka kwa ajili ya kuendeleza matawi, faida zote za ubingwa na zawadi inachukua timu, usajili anafanya yeye, mishahara analipa yeye, biashara zote ambazo zingeanzishwa katika kipindi hicho 25% ya faida ingechukua Yanga.”

“Baada ya miaka 10 klabu ingerudi kwa wanachama lakini tukaona haifai na tukabeza lakini hatukuwa na njia mbadala, ametoka tunaanza kulalamika tunataka arudi.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here