Home Kimataifa Luis Monti, mwanadamu pekee aliyecheza kombe la dunia mataifa mawili tofauti

Luis Monti, mwanadamu pekee aliyecheza kombe la dunia mataifa mawili tofauti

11876
0
SHARE

Hakuna bahati kubwa kama kucheza michuano ya kombe la dunia, ndio maana Diego Maradona amekiri kwamba jasho la zile siku 30 katika michuano hiyo ni jasho tamu zaidi katika soka kwa mwanaume.

Lakini kama kuna bahati katika kombe la dunia baasi Muargentina mwenzake Maradona aitwaye Luis Monti alibahatika zaidi kwani huyu ndio alikuwa mwanadamu pekee kuwahi kushiriki kombe la dunia kwenye mataifa mawili tofauti.

Monti ana asili ya Argentina ambako alizaliwa huko mwaka 1901 na kuanza soka lake katika vilabu vya Huracan, Boca Juniors na baadae San Lorenzo akitajwa kama kati ya kiungo mkabaji bora kuwahi kutokea Argentina.

Mashindano ya kombe la dunia 1930 pale nchini Uruguay yalimpa heshima Monti katika hatua za mwanzo, aliisaidia Argentina kuifunga Ufaransa kabla ya kuwapiga bao 6-1 Mexico na kisha wakaipiga Chile bao 3-1.

Nusu fainali alifunga moja ya bao walipoifunga USA mabao 6-1, lakini fainali walikutana na Uruguay na half time tu Argentina akala 2-1, na hadi baada ya dakika 90 Argentina walikufa kwa bao 4-2.

Baada ya mchezo huu inadaiwa kwamba Monti pamoja na wachezaji wengine walianza kupokea vitisho kutoka kwa mashabiki mbalimbali wa Argentina wakitishia maisha yao na hii ikawafanya waishi kwa mashaka.

Wakati jambo hili linatokea ikaja ofa kutoka nchini Italia, ambako aliahidiwa $5000 kwa mwezi pamoja na gari. Ofa hii ndio ilihitimisha uraia wa Monti katika nchi ya Argentina kwani aliamua kusepa.

Alipofika Italia Monti aliichezea Juventus na uhamisho huu ukiwa na ushawishi mkubwa kutoka kwa mtawala wa Italia kipindi hicho Benito Mussolini na lengo lake haswa ni Monti kuwasaidia kutwaa kombe la dunia 1934 ambalo Italia walikuwa waandaaji.

1934 Argentina ambako ndiko aliondoka Monti waliondolewa na Sweden katika siku ambayo Monti alikuwa akilichezea taifa lake jipya la Italia na kuifunga USA kwa mabao 7-1.

Robo fainali Italia akakutana na Hispania na kutoka sare ya 1-1 na mchezo kuamuliwa kurudiwa ambapo baada ya marudiano Italia walifudhu kwenda nusu fainali kwa bao la Guissepe Meaza.

Inadaiwa mchango mkubwa wa Mussolini na figisu ziliifanya Italia kuingia fainali na wachezaji wa timu ya taifa ya Italia walipewa onyo na Mussolini akiwaambia inabidi washinde mchezo huo ama wafe.

Italia walikutana na Czechoslovakia katika fainali huku Italia wakipewa nafasi kubwa kushinda lakini hadi dakika ya 75 walikuwa nyuma kwa bao moja kwa nunge mbele ya wapinzani wao walioonekana vibonde.

Dakika ya 81 Italia walisawazisha bao hilo kupitia kwa Raimundo Orsi kabla ya Angelo Schiavo kuipatia Italia bao la pili ambalo lilimfanha Monti kubeba kombe la dunia akiwa katika taifa lake lingine.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here