Home Kimataifa Floyd “Money” Mayweather aendelea kuwapoteza Messi na Cr7

Floyd “Money” Mayweather aendelea kuwapoteza Messi na Cr7

12035
0
SHARE

Jariba maarufu la masuala ya biasha na kipato la Forbes limetoa orodha mpya ya wanamichezo ambao wanalipwa pesa nyingi, tathmini hii imefanywa kwa siku za karibuni kuanzia June 2017 hadi June 2018.

Jina la mwanamasumbwi Floyd Mayweather bado linaendelea kushika namba moja katika orodha ya wanamichezo walioingiza mkwanja mrefu kwa kipindi hiki akiwa amepewa kiasi cha $285m.

Sababu kubwa ambayo imemfanya Mayweather kuwa tajiri kiasi hiki ni pambano lake na Conor McGregor ambalo lilimfanya kuwa mwanamichezo wa 3 kuwahi kutengeneza $1b katika mchezo mmoja huku akilipwa karibia $275m katika pambano hilo.

Manguli wawili katika soka Lionel Messi na Cristiano Ronaldo ndio wanaomfuatia Mayweather, ambapo Messi yuko nafasi ya pili akiwa amelipwa $111m katika muda huu wa miezi 12.

Baada ya Messi yupo Cristiano Ronaldo ambaye hadi sasa anawaza mkataba mpya ndani ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo kwa kipindi hiki cha June 2017 hadi June 2018 amepokea $108m ikiwa ni pungufu ya $3m kutoka alipo Messi.

Aliyekuwa mpinzani mkubwa wa Mayweather, bondia Conor McGregor anashikilia nafasi ya nns akiwa na $99m, huku mchezaji ghali zaidi duniani Neymar akiwa katika nafasi ya 5 na kiasi cha $90m.

LeBron James yuko nafasi ya 6 na $85.5m, huku mcheza tennis Rodger Federer akiwa nafasi ya saba na $77.2m, Stephen Curry yuko nafasi ya nane na $76.9m, huku nafasi ya 9 ikienda kwa mcheza baseball Matt Ryan $67.3m na ya 10 ni Matthew Stafford $59.5m

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here