Home Kitaifa Yanga ina mpango kuziba nafasi ya Manji?

Yanga ina mpango kuziba nafasi ya Manji?

10723
0
SHARE

Hivi karibuni Yanga itafanya mkutano mkuu lakini wanachama na wapenzi wa klabu hiyo wanatamani kujua kupitia mkutano huo watapata viongozi wapya kuziba nafasi ya aliyekuwa mwenyekiti wao Yusuf Manji ambaye alijiuzulu tangu mwezi Mei 2017.

Nafasi nyingine ambazo zipo wazi ni za wajumbe wa kamati ya utendaji (Hashim Abdalla na Salum Mkemi) ambao wamejiuzulu hivi karibuni.

Kaimu mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga amesema mkutano mkuu ujao utakuwa na lengo la kuwaeleza wanachama matatizo yanayoikabili timu, kuhusu uchaguzi wa kuzipa nafasi zililizo wazi utatangazwa baadaye.

“Ukiangalia katiba yetu inapozungumzia mwenyekiti anapokuwa ameondoka madarakani kwa kujiuzulu, katiba inasema makamu atachukua nafasi hiyo mpaka mkutano mkuu unaofuata kwa ajili ya kujaza nafasi hiyo.”

“Pamoja na hayo, katiba ina mapungufu mengi sana. Ukizungumzia mkutano unaofuata maana yake kwenye mkutano huu ujao wa Juni 10 tufanye uchaguzi, lakini nadhani malengo yalikuwa ni kwa ajili ya nafasi nyingine ndogondogo kwa sababu unawezaje kufanya uchaguzi kwa nafasi kubwa na siku hiyo ukafanya mkutano mkuu wa wanachama?

“Kwa hiyo sisi tumeona ni afya kufanya mkutano mkuu wa wanachama ili tuwaeleze matatizo yaliyojitokeza, hata kama kuna kiongozi yoyote anaingia kwenye nafasi hiyo awe anajua nini kinatakiwa kufanyika baada ya kuchaguliwa, vinginevyo hatakuwa na taarifa yoyote.”

“Tutaenda kwenye mkutano mkuu wa wanachama, tutajadili baada ya hapo maelekezo ya kuja kujaza nafasi ya mwenyekiti tutatangaza muda ambao pia upo ndani kwa mujibu wa katiba na tutajitahidi kufanya muda mfupi ili ushiriki wa ligi kuu wa msimu ujao usiwe na matatizo hasa katika masuala ya usajili.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here