Home World Cup Wajue makinda wasioimbwa watakaosumbua kombe la dunia

Wajue makinda wasioimbwa watakaosumbua kombe la dunia

11205
0
SHARE

Elizabeth lyavule

zimesalia siku tisa tu mataifa 32 yakianza kuoneshana ubabe kombe la dunia, huku macho ya wengi wakingojea kumuona Marcus Rashford na Uingereza, Marco Asensio na Hispania, Paul Dybala wa Argentina na wengine wengi, jaribu kuwafumbia macho hawa tuliowazoea na uwacheki makinda hawa tusiowajua sana na kuwasifu uwezo wao kule Urusi.

Hirving Lozano raia wa Mexico. Alianza maisha yake ya soka kama mshambuliaji nchini kwao Mexico akiwa na klabu ya Pachuka, msimu wake wa kwanza alifunga magoli 18 ndani ya michezo 37 aliochezea klabu yake hivyo maskauti wa timu ya PSV nchini Uholanzi walimuona wakamsajili na akiwa PSV amemaliza msimu akiwa ni mfungaji bora wa klabu magoli 17 na mfungaji namba tano wa ligi ya uholanzi pia alifanikiwa kutoa pasi za mwisho zilizozaa magoli 9 kubwa zaidi kaisaidia PSV kuwa mabingwa wa uholanzi (eredvisie).

Ana uwezo mkubwa wa kupiga mipira iliyokufa, ana krosi nzuri na katika umri wake wa miaka 22 aliitwa timu ya taifa Mexico na mchezo wake wa kwanza ilikua mwezi wa pili mwaka 2016 dhidi ya Senegal alifanikiwa kutoa pasi ya goli katika mechi hiyo. Ana magoli 7 katika michezo 26 aliyoichezea nchi yake moja akiifunga timu ngumu ya ubeligiji mwezi wa 11 mwaka 2017 katika sare ya goli 3-3. Ana uhakika wa namba Mexico tuone ataunda vipi ushirikiano na wenzie kuifanya nchi yao ifike mbali mwaka huu kule Urusi.

Lucas Torreira wa Uruguay ni kinda mwenye miaka 22 anaetizamiwa kuwa na mashindano mazuri ya kombe la dunia Urusi. Anacheza kama kiungo mkabaji na sasa yupo katika klabu ya Sampdoria nchini Italia, msimu uliokwisha amecheza michezo 33 ya ligi ya Italia “seria a” ametengeneza nafasi 33 za kufunga, akiingilia mpira kwa mpinzani (interception) mara 67 pia akifanikiwa kumpora mpira mpinzani (tackling) mara 66 si kitu kidogo kwa umri wake. Kwa takwimu hizo haitakua ajabu kumuona akiunda kikosi cha kwanza na wakali wengine kama Diego Godin, Suarez, Edson Cavan nakuifikisha mbali nchi yake katika mashindano hayo.

Aleksandr Golovin wa Urusi. Akiwa ni mwenyeji kinda huyu mwenye miaka 22 atapambana vilivyo kuiokoa nchi yake kukwepa aibu yakutoka mapema, anacheza katika klabu ya CSKA Moscow ya urusi na ni mmoja kati ya wachezaji waliobeba kombe la Ulaya la vijana chini ya miaka 17 mwaka 2013,

kinda huyu ni kiungo wa kati anaeweza kuunganisha timu kati ya ulinzi na ushambuliaji (box to box midfielder) huku akisifika kwa uwezo mkubwa wa kukokota mpira, kutoa pasi nzuri na kukaa na mpira bila adui kumpokonya.

Amecheza mechi 38 mashindano yote msimu wa 2017-2018 akafunga magoli 7, akatoa pasi za kufunga 4 si kitu cha kubeza kwa umri wake.

Ismaila Sarr raia wa Senegal. Kinda huyu wengi wanamlinganisha na Sadio Mane na wanamtabiria kufanya vizuri kuliko Sadio Mane akikomaa mana ndio kwanza ana miaka 22 tu.

Anacheza nafasi ya ushambuliaji kutokea pembeni huko Ufaransa katika klabu ya Rennes na msimu wake wa kwanza alikua na goli 5 pasi za mwisho zilizozaa magoli 5 katika michezo 22 aliyoanza huku 2 akitokea benchi. Akiwa na Senegal mwezi wa 9 mwaka 2016 alicheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Namibia akitokea benchi kuchukua nafasi ya Sadio Mane.

Kwasasa kashacheza michezo 10 nakufanikiwa kupata magoli 2. Ataungana na washambuliaji wengine kama Mame Biram Diouf, Maussa Sow, Diafra Sakho na Sadio Mane kuhakikisha wanaiwakilisha vizuri Senegal na Africa kiujumla wafike mbali.

Cristian Pavon kinda kutoka Argentina. Winga huyu hategemewi sana kupata nafasi kutokana na upinzani wa nafasi anayocheza kujaa wachezaji wazuri wenye vipaji kama Angel Di Maria, Paul Dybala na mfalme Leonel Messi.

Anacheza nchini kwao Argentina katika klabu ya Boca Junior,kawa na msimu bora ulopita akiifungia klabu yake magoli 6 nakutoa pasi 11 za mwisho zilizozaa mabao nakumfanya kocha Sampaoli kumuita kikosi cha wachezaji 23 watakaoiwakilisha nchi kombe la dunia,

aliichezea Argentina dhidi ya Urusi mwaka uliopita na kufanikiwa kutoa pasi iliozaa goli pekee lililofungwa na Sergio Kun Aguero katika ushindi wa 1-0 waloupata pia alitoa pasi kati ya magoli mawili katika mchezo wa kirafiki waliopoteza dhidi ya Nigeria.

Macho ya vilabu vyote vikubwa barani Ulaya yatakua Urusi kucheki vipaji kama hivi na haitakua ajabu kusikia wameenda timu kama Manchester utd, Arseno na Napoli pindi dirisha la usajili litakapofunguliwa majira haya ya kiangazi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here