Home World Cup Timu ya kwanza kufika Urusi kwa ajili ya World Cup hii hapa

Timu ya kwanza kufika Urusi kwa ajili ya World Cup hii hapa

12551
0
SHARE

Kuna kale kamsemo waswahili husema kutangulia bar sio kulewa. Lakini huwa waswahili hawa hawa mimi wananichanganya akili. Wakishakwambia hivyo ukizuga zuga wanakwambia chelewa chelewa utakuta mwana si wako.

Tena wapo wale wanaojiita Wahenga wanasema kwamba haraka haraka haina baraka, lakini ukijifanya mtaratibu saa watakung’ong’a kwa kebehi kwamba ngoja ngoja huumiza matumbo.

Wapersia wa Iran wao wameona wasizungukeeee sanaaa. Wao mapemaa washatimba Urusi. Hawana mambo mengi. Wao wamefuata kombe lao tu. Hawana tatizo na mtu.

Naam.. Timu ya taifa ya Iran wao tayari washatia maguu katika ardhi ya Putin kwa ajili ya mtanange wa Kombe la dunia.

Wao wameona hakuna haja ya kupoteza muda na wamefika mapemaaa kabisa ili kuisoma hali ya hewa halafu hapo baadae wausome mchezo. Wanajiamini na wanajua fainali ina wahussu na hawaachi kitu kabisa. Wametumwa ubingwa . Hawajenda kuuza sura au kushiriki. Wapo kazini. Hawarembirembi mambo. Wao wanachokijua ni kwamba Nyota njema huonekana asubuhi.

Wameawaacha wajerumaani waendelee kujadili kwanini Sane ameachwa na Wabrazil waendelee kumpongeza Fred kwenda Man United lakini waomkifika tu wakabidhiwe ubingwa wao.

Kocha mkuu wa taifa hilo Bwana Carlos Queroz ametoa tahadhari mapemaa. Amesema wapinzani wao watakiona cha mtema kuni. Afe mfugaji lakini lazima ng’ombe afike mnadanai. Ndio. wamesema sahauni kabisa kuhusu alama za bwerere.

Kocha huyo amesema wao watagawa dozi wala haakuna masihara kabisa. Wamefika mapema ili warilaksi na kuwaondoa wenge wachezaji wao.

Iran walikuwa timu ya kwanza ya Asia kukata tiketi ya bombadia kwenda Urusi. Hata hivyo hii ni kwa mara yao ya 5 wanakwenda katika mashindano ya Kombe la dunia.

Iran walifikia uwanja wa Ndege wa Vnukovo mapema hivi leo huku wakijiandaa na Mpambano wao wa kwanza dhidi ya Morocco june 15 katika uwanja wa St Petersburg.

Iran wamefikia katika kambi ya Lokomotiv Bakovka ambapo ndipo watapumzikia na kupanga mipango yao.

Mwiisho kabisa Kocha wao mkuu amewatakia kila mshiriki Kombe la Dunia Jema.

Mambo yapo mbio mbio ndugu zangu. Bado siku 8 tu. Ushajipatia king’amuzi cha Dstv mapema? Hebu changamkia fursa kama ndugu zako wa Iran. Usibabaishwe mambo yote yapo Dstv, kama Sio Dstv POTEZEA TU.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here