Home Kitaifa Sanga kuhusu wanaojiuzulu Yanga “hatutakiwi kukimbia mapambano”

Sanga kuhusu wanaojiuzulu Yanga “hatutakiwi kukimbia mapambano”

8771
0
SHARE

Hivi karibuni kuna baadhi ya wajumbe wa kamati ya utendaji ya Yanga wameamua kujiuzulu kutokana na sababu mbalimbali.

Salum Mkemi ni miongoni mwa wajumbe waliojiuzulu na kusema matokeo mabovu ya Yanga ndio sababu ya yeye kujiuzulu.

Ukiachana na Mkemi, Hashim Abdallah pia alitangaza kujiuzulu hivi karibuni na kusema aliingia kwenye uongozi akiwa na lengo la kuitoa Yanga sehemu moja kwenda nyingine ikiwa ni kubeba vikombe, kujiendesha yenyewe bila kutembeza bakuli lakini kwa muda wa miaka miwili aliokuwepo kwenye uongozi amefeli ndio maana amekaa pembeni.

Sanga amesema ukiwa vitani hutakiwi kukimbia mapambano, unatakiwa kupambana hadi mwisho.

“Tupo kwenye vita hatutakiwi kukimbia mapambano, tunatakiwa kupambana hadi mwisho halafu tuwaambie waliotuchagua tumefikia hapa, wao ndio watakuwa na maamuzi tufanye nini baada ya kufika hapo na baada ya hapo kitatokea hicho kinachotakiwa kutokea kwa maslahi mapana ya Yanga.”

“Ukiangalia sababu ambazo zimetolewa ambazo zimekuwa wazi na naweza kuzizungumzia, kuna mjumbe amejiuzulu na amesema ameona kwamba tumeishia nafasi ya tatu kwenye ligi kwa hiyo anawajibika.”

“Nimeangalia nimeona kila mwaka hata vilabu vingine vingekuwa vinafanya mabadiliko ya uongozi kwa sababu havijamaliza katika nafasi ambazo walijiwekea malengo.”

“Waliowachagua wanajua kwa nini wamesema vile lakini wao ndio watakuwa na hoja nyingi za kuhoji kwa nini viongozi wao wamejiuzulu.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here