Home Kitaifa Kocha wa Mtibwa kuhusu ubora wa Dilunga msimu huu

Kocha wa Mtibwa kuhusu ubora wa Dilunga msimu huu

9525
0
SHARE

Hassan Dilinga alitangazwa kuwa mchezaji bora wa mashindano ya Azam Federation Cup 2018 baada ya kuisaidia timu yake kushinda ubingwa wa mashindano hayo.

Dilinga amewahi kucheza Yanga, Ruvu Shooting amefanya vizuri msimu huu akiwa na Mtibwa Sugar kwa kuisaidia kumaliza ligi katika nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi kuu.

Kocha wa Mtibwa Sugar Zubery Katwila amezungumzia kilichombadilisha Dilunga na kuonekana bora msimu huu.

“Dilunga ni mchezaji anaeweza kubadili matokeo uwanjani wakati wowote, mbunifu anaweza kufanya chochote na anaunganisha mbele na katikati. Ni mchezaji wa aina yake na kwenye timu yangu namtumia kama mchezaji muhimu ambaye huwa namfanya awe huru afanye anachotaka.”

“Ni mchezaji mzuri, hapo katikati alipokuwa kwenye timu nyingine alikuwa anajitahidi kurudisha kiwango chake lakini hakukifikia.”

“Kuna wakati nilimuhitaji lakinisl sikufanikiwa kumpata, wakati huo nilikuwa kocha msaidizi Meck ndio alikuwa kocha mkuu. Sasa hivi mimi ndio kocha mkuu nimejitahidi hadi nimempata kwa sababu nilikuwa najua ana kitu gani na Mtibwa tunaweza kunufaika nae.”

“Nilimwambia wewe utatusaidia badae na kweli mafanikio anayaona hana jibu la kunipa zaidi ananipa tu pongezi kwa mafanikio anayopata.”

Dilunga amekuwa mfungaji bora kwa upande wa Mtibwa Sugar kwenye kombe la ASFC akiwa na magoli manne magoli mawili nyuma ya mungaji bora wa mashindano Habib Kyombo aliyefunga magoli sita.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here