Home World Cup Man City yatisha kombe la dunia

Man City yatisha kombe la dunia

8442
0
SHARE

Na: DANIEL S.FUTE

ZIKIWA zimesalia takribani siku kumi kuanza kwa fainali za Kombe la Dunia, tayari tumeweza kuona vikosi mbali mbali ambavyo vitaenda kuwakilisha vyema mataifa yao katika mchezo wa Soka.

Lakini kupitia vikosi hivyo wapo wachezaji kadha wa kadha ambao wanacheza Soka la kulipwa katika klabu mbali mbali ambao ni waajiri wao.

Wachezaji wengi wanaoitwa katika timu zao za taifa na makocha wao, huwa wanaangaliwa sana katika ubora ambao wanaonesha katika klabu zao.

Klabu ya Manchester City kutoka katika Ligi kuu England, ndio imekuwa klabu pekee kupeleka wachezaji wengi katika fainali za Kombe la Dunia 2018.

Man City imeweza kutoa wachezaji 16, ambao wameenda kuungana na mataifa yao kwaajili ya fainali hizo zitakazoanza wiki ijayo.

Hii inaonyesha ni jinsi gani klabu hii ilivyoundwa vyema katika msimu wa Ligi kuu uliopita kupitia kocha wao mkuu, Pep Guardiola.

Na hawa ndio wachezaji 16 ambao watasafiri na mataifa yao katika fainali hizi za Kombe la Dunia:

Vincent Kompany, Danilo, Ederson, Stones, Sterling, Walker, Delph, Benardo Silva, David Silva, De Bruyne, Otamendi, Fernandinho, Gundogan, Gabriel Jesus, Kun Aguero na Benjamin Mendy.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here