Home Kitaifa Mkemi amejivua uongozi Yanga

Mkemi amejivua uongozi Yanga

10446
0
SHARE

Baadhi ya viongozi wa Yanga wameendelea kuikimbia klabu hiyo kwa kujiuzulu nafasi zao za uongozi.

Mjumbe wa kamati ya utendaji Yanga Salum Mkemi ambaye mara kadhaa alihusishwa kuikacha Yanga leo ameandika waraka ambao umesambaa kwenye mitandao akitangaza kupisha nafasi kwa watu wengine kuongoza.

Ujumbe wa Mkemi kujiuzulu uasomeka hivi: Kusema kweli viongozi hatukwepi lawama hizi, kwa hakika tumepata aibu kubwa.

Nikiwa kama kiongozi napaswa kuwajibika kwa hili ni hatua nzuri ya kupisha mawazo mapya kwa wanachama wengine kuongoza timu na kutupeleka mbele.

Pia ningependa kuwashauri viongozi wenzangu wajitathimini na ikibidi nao waachie ngazi ufanyike uchaguzi mkuu kwa pamoja tupate viongozi wapya kabla msimu mpya haujaanza.

Napenda kuomba samahani kwa wote niliowakwaza na nimesamehe wote walio nikikwaza.

Naomba kutamka rasmi mimi Salum Mkemi
najaiuzulu nafasi zangu zote za uongozi ndani ya klabu yangu pendwa Young Africans Sports Club ‘YANGA’ kuanzia tarehe ya leo 03/06/2018.

Nawatakia kila la heri viongozi wenzangu waliobaki na kuwataka radhi tena wanachama, wapenzi na mashabiki wa Yanga kwa matokeo mabovu tuliyopata naomba tusamehane.

Nawashukuru kwa muda mlionipa kuiongoza klabu hii kubwa Afrika naomba Kuwajibika kwa kujiuzulu.

Wenu mwanachama mwenzenu mtiifu.

Salum Mkemi.

NIMENG’ATUKA

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here