Home Dauda TV Kuna uhusiano kati ya marehemu Shose na ASFC? “Nimetokanae mbali sana”-Henry

Kuna uhusiano kati ya marehemu Shose na ASFC? “Nimetokanae mbali sana”-Henry

10779
0
SHARE

May 27, 2017 Simba ilishinda ubingwa wa ASFC baada ya kuifunga timu iliyopanda daraja (Mbao FC) kwenye mchezo wa fainali lakini siku moja baadaye Simba ilipata pigo kwa kumpoteza shabiki wake Shose Fidelis aliyefariki kwa ajali ya gari wakati wanatoka Dodoma kuelekea Dar.

Ni mwaka mmoja sasa tangu Shose afariki, lakini baada ya fainali ya ASFC June 2, 2018 mchezaji wa zamani wa Simba Henry Joseph baada ya kuisaidia Mtibwa kuchukua ubingwa huo alivaa t-shirt yenye picha ya Shose ikiwa imeandikwa ‘R.I.P SISTER SHOSE FIDELIS’.

Henry Joseph amesema ameamua kufanya hivyo ili kumuenzi Shose ambaye alifariki baada ya fainali ya kombe la ASFC ndio maana ameimevaa baada ya mchezo wa fainali.

“Ni dada yangu ambaye nimetokanae mbali sana, alifariki kwenye fainali baada ya Simba kutwaa ubingwa kwa hiyo namkumbuka sana alikuwa mtu wa kipekee na kila mtu anajua.”

“Hii nimevaa kwa niaba ya watu wote wa Makongo Secondary kwa sababu tumesoma pamoja.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here