Home Kimataifa #RoadToRussia, mkosi wa goli 3 unavyoitafuna “Three Lions” kombe la dunia

#RoadToRussia, mkosi wa goli 3 unavyoitafuna “Three Lions” kombe la dunia

9742
0
SHARE

Usiku wa leo timu ya taifa ya Uingereza itakuwa katika uwanja wao wa nyumbani kuwakaribisha Nigeria katika kujiandaa na kombe la Dunia, ni mchezo muhimu kwa pande zote mbili kujiweka sawa kabla ya kuelekea nchini Urusi.

Kuna jambo la ajabu kuhusu timu ya taifa ya Uingereza ambalo mashabiki wao wengi mitandaoni wanalijadili, bao 3. Uingereza wanaomba chonde chonde usiku wa leo wasiwafunge Nigeria magoli 3.

Rekodi zinaonesha kwamba timu ya taifa ya nchini Uingereza ilipata matokeo mabovu katika kombe la dunia baada ya kupata ushindi wa mabao 3 katika mechi ya mwisho ya kujiandaa na kombe la dunia waliyocheza Wembley kwenye misimu mitatu mfululizo iliyopita.

Kombe la dunia 2014, mchezo wa mwisho wa maandalizi ya kombe la dunia kwa Three Lions mwaka 2014 ilikuwa dhidi ya Peru katika dimba la Wembley, katika mchezo huu Three Lions waliibuka kidedea kwa mabao 3-0.

Daniel Sturridge, Gary Cahill na Phil Jagielka walikuwa wauaji katika mchezo huu, lakini walipokwenda katika michuano ya kombe la dunia nchini Brazil, Uingereza walishuhudia wakiondolewa katika hatua ya makundi.

Kombe la dunia 2010, mwaka 2010 nao Uingereza mchezo wao wa mwisho kujiandaa na kombe la dunia ulipigwa Wembley, safari hii walicheza dhidi ya Mexico na kuibuka kidedea kwa mabao 3-1.

Ledley King, Peter Crouch na Glen Johnson waliiua Mexico, baada ya hapo Waingereza wakakwea pipa na kwenda zao nchini Afrika Kusini walipofika kwa Madiba wakadharilika hatua ya 16 bora kwa kupigwa na Ujerumani bao 4-1.

Kombe la dunia 2006, Steven Gerrard, John Terry na Peter Crouch waliifunga Hungary bao 3-1 mwaka 2006 katika mchezo wa mwisho wa Uingereza kabla ya kombe la dunia na safari hii mchezo ulipigwa Old Traford.

Walipokwenda Ujerumani walisogea sogea hadi robo fainali, lakini Wareno wakawaondoa kwa matuta huku Wayne Rooney akipewa moja ya kadi nyekundu maarufu zaidi katika michuano hii.

Usiku wa leo ni Uingereza na Nigeria pale Wembley, je kitakachotokea kitaathiri safari ya Urusi?

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here