Home Kimataifa #RoadToRussia, dakika 3 tu zavunja rekodi ya mauzo ya jezi ya Nigeria

#RoadToRussia, dakika 3 tu zavunja rekodi ya mauzo ya jezi ya Nigeria

16128
0
SHARE

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, jezi ya timu ya taifa ya Nigeria imevunja rekodi ndani ya dakika chache tu tangu kampuni ya kutengeneza vifaa ya Nike kuiweka sokoni officialy.

Dakika tatu tu baada ya jezi hizo kuwekwa sokoni inasemekana mamia ya wakazi jijini London walikaa katika foleni nje ya duka la Nike kusubiri jezi hiyo na wengine kununua kupitia Website ya Nike na kuzimaliza katika muda huo mfupi.

Kabla ya Ijumaa ya leo ambayo ndio siku rasmi ya jezi hiyo kuanza kuuzwa, inadaiwa kwamba Nike walishapokea oda ya takribani jezi milioni 3 kutoka kwa wateja wao dunia nzima.

Sio tu jezi official ya timu bali pia jezi ya ugenini watakayoitumia Nigeria katika michuano hiyo imekwisha huku pia jezi ambayo Nigeria watatumia katika mazoezi wakati wa michuano hiyo imekwisha.

Chama cha soka nchini Nigeria kilihakikisha jezi hii inauzwa original tu, lakini pia uwepo wa order nyingi ya jezi hii iliifanya Nike kuchelewa kuitoa na sasa ukiitaka itakubidi kutoa £64.95 ili kuipata.

Msanii maarufu wa Nigeria Wiz Kid pamoja na nyota wa Arsenal Alex Iwobi wametumika kwa kiasi kikubwa kuifanyia promo jezi hii ambayo kwa sasa inazungumziwa mno ulimwenguni.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here