Home World Cup Miamba hatari iliyowahi kugaragazwa Kombe la dunia

Miamba hatari iliyowahi kugaragazwa Kombe la dunia

8733
0
SHARE
Brazil 1982

Ukiachilia mbali mafanikio makubwa walio nao vijana wa Seleção ya kushinda mataji matano ya kombe la dunia lakini Brazil bado ni taifa ambalo limezalisha kizazi bora cha dhahabu katika michuano ya kombe la dunia wakiongozwa na Pele. Brazil kunako 1982 walikuja na kizazi bora kabisa katika historia ya soka lao. Tuanzie hapa kwa Zico, Falcão, Socrates.

Utamuaminish vipi mtu kwamba kikosi hiki kilitoka patupu. Vijana wa Telê Santana walifanikiwa kufuzu hatua ya makundi kule nchini Spain. Waliongoza kundi lao wakiwa na magoli 10 mkononi baada ya michezo 3. Brazil ilikuwa na kiungo bora kuwahi kutokea miaka ya 1970 mpaka 1989 Ajulikanae kama Falcao.

Falcao miaka 1980 alipachikwa jina la Mfalme wa 8 wa Roma. Mzee Radamel Garcia aliamua kumpa mtoto wake jina la Falcao ambaye ndiye Radamel Falcao wa sasa ili kumuenzi. Falcao aliwahi kuwa mchezaji bora na wa ghali zaidi duniani kwa miaka ile. Alisaidia na Eder, pamoja na Luizinho na Oscar akiwa mbavu za kulia. Brazil walipangwa kundi moja na Italia pamoja na Argentine.

Huku Serginho akiwa Brazil, Kule Rossi wa Italy na Argentine wakiwa na Maradona. katika kundi lile Maradona alishindwa kupenya ngome ya waitaliano chini ya usimamizi wa Gaetano Scirea na Claudio Gentile. mchezo uliofuata Brazil waliifumua Argentine mabao matatu kwa nunge huku Diego maradona akitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kupigana uwanjani.

Mchezo wa mwisho ulikuwa kati ya Italia na Brazil kutafuta nani atasimama juu ya kundi na kusonga mbele. Italia waliibuka kidedea kwa mabao 3-2 Paolo Rossi akipiga hat trick. Mchezo huu unasemekana ni mchezo wa kuvutia zaidi katika kombe la dunia.

Uholanzi 1974

Miaka ya hapo awali Ajax waliibuka kuwa miamba ya ulaya baada ya kutwa kombe la Ulaya mara tatu. Rinus Michels aliamua kuchukua mfumo ule wa Ajax wa Total football (Timu nzima kukaba kwa pamoja) kule Ujerumani magharibi.

Uholanzi iliongozwa na Legendi Johan Cruyff. Falsafa yao ya kukaba kama nyuki, kupiga pasi nyingi nakushambulia kama hawataki ulivutia wengi. Walijitahidi kiasi cha kufika fainali ambapo walikutana na wenyeji ujerumani Magharibi. Cruyff alifunga bao la penati lilisababishwa na Johan Neeskens.

Lakini kisicho riziki hakiliki mabao ya Paul Breitner na Gerd Müller yaliondoa ndoto ha wadachi kutwaa kombe la dunia. Cruyff alipoga chenga murua kabisa ambayo ilipewa jina lake katika mchezo wao dhidi ya Sweden.

Ureno 1966

Kombe la dunia la mwaka 1966 lilifanyika nchini England. Portugal walikuwa wakipewa nafasi kubwa zaidi katika kunyakua kinyago cha Jules Rimet. Ureno ilijumuisha mastaa wakubwa kutoka Benfica, ambao walitwa ubingwa European Cup in 1961 and ’62 chini ya legendari Hungaria kocha Béla Guttmann ambaye anajukikana zaidi duniani kwa mfumo wa Cattenaccio.

Mfungaji bora wa ureno winga Eusébio, aliibuka mfungaji bora wa michuano ile kwa mabao 9. Walisshinda michezo yote mitatu ya makundi ikiwemo kochapo ilichotoa kwa mabingwa watetezi Brazil. England walotwaa ubingwa huo kwa kuifunga Ureno kwa mabao 2-1

Brazil 1950

Hatutakuwa wawazi kama tutiasema vibaya Brazil iliyopigwa na Ujerumani magoli 7. Haikuwa na kikossi cha kutisha sana wala
hakuna aliyeshanga Brazil kuukosa ubingwa huo. Mwaka 1950 Brazil waliandaa mashindano ya kombe la dunia. Hii inaonesha ni aibu kubwa ma fedheha kubwa katika maisha yao ya soka.

Wakati huo Brazil walikuwa wanavaa fulana zao nyeupe kabla hawajabadilisha na kuvaa njano na buluu mwaka 1953. Brazil iliongozwa na ademir pamoja na Zizinho. Brazil walihitaji sare dhidi Uruguay ili kufika hatua ya fainali. Wakati huo kombe la dunia lilikuwa na makundi mawili tu. Friaca aliwapa Brazil bao la kwanza kabla Juan Schiaffino hajasawazisha.

Muuaji wa Brazil ni Alcides Ghiggia aliyewapa Uruguay bao la ushindi na kufuta kabisa ndoto za wabrazil.

Hungary 1954

Baada ya kuifumua England 6-3 katika uwanja wa Wembley mwaka mmoja uliopita Hungary ilijizoelea umaarufu mkubwa duniani miaka ya 1954 hasa kagika micuano ya kombe la dunia lililofanyika nchini Switzerland.

Hungary ilikuwa na wachezJi bora kama Ferenc Puskás, Nándor Hidegkuti, Sándor Koscis, Gusztáv Sebes’ ‘Magical Magyars’. Katika micchezo miwili ya makundi walishinda magoli 17, ikiwemo ushindi wa mabao 8-3. Ubora wao ulimalizwa na Ujerumani kwa mabao 3-2.

Italia 1990

Miaka ya mwaka 1990 walikuwa waandaji wa kombe la dunia. Walipewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa.

Wakati ule Serie A ilitawala sana michuano mikubwa ya ulaya. Ilikuwa na wachezaji bora duniani kama vile Paolo Maldini, Franco Baresi, Roberto Baggio pia alikuwa mshambuliaji hatari wa Juventus Salvatore ‘Toto’ Schillaci amabaye alitwaa kiatu cha dhahabh kwa kufunga magoli 6.

Italia walifanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali na kufungwa na Argentine ambao nao walipoteza kwa miamba ya ujerumani magharibi katika hatua ya fainali.

imeandaliwa na Privaldinho. Unaweza pia kunifollow Instagram kwa jina hilo hilo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here