Home Kimataifa Siasa ya Uk vs Russia kuiingiza Chelsea katika anguko

Siasa ya Uk vs Russia kuiingiza Chelsea katika anguko

11748
0
SHARE

Mkwaruzano wa kisiasa baina ya mataifa mawili ya Russia na Uingereza unaiweka mahala pabaya klabu ya Chelsea na maendeleo yake.

Mmiliki wa Chelsea bwana Roman Abramovich ambaye ni raia wa Russia 🇷🇺 leo amesitisha rasmi mpango wa kujenga uwanja mpya wa Stamford Bridge ambao ungeweza kuchukua watu 60,000 – akitoa sababu kwamba hakuna mazingira mazuri ya uwekezaji nchini Uingereza kwa sasa.

Abramovich ambaye ni mshirika wa karibu wa Rais wa Urusi Vladimir Putin, alinyimwa visa mpya wa UK tangu mwezi wa 4 na hivyo kumfanya akose kuhudhuria mechi ya fainali ya FA Cup vs Manchester United.

Uingereza na Russia zimekuwa kwenye mikwaruzano ya muda sasa upande wa masuala ya kisiasa chini ya viongozi wao PM Theresa May na Rais Putin.

Juzi Roman Abramovich alipata uraia wa Israel 🇮🇱 ili aweze kupata visa ya UK kiurahisi lakini bado akawekewa ngumu kwenda UK kuendelea na kazi – jambo ambalo leo limepelekea kusitisha mipango yake ya uwekezaji katika klabu ya Chelsea ambayo anaimiliki.

Chelsea ambao walikuwa wanajiandaa kwa ajili ya msimu ujao – wana mtihani wa kumalizana na Conte, na kumuajiri kocha mpya Maurizio Sarri ambaye atasimamia usajili. Mambo haya sasa yanaonekana yatapata ugumu kutokana na hali ilivyo baina ya mmiliki Roman Abramovich na serikali ya UK.

Ikumbukwe kwamba wakati haya yanamkuta Roman Abromovich pia timu yake haipo katika michuano ya Champions League, na hii pia linaweza kuwa tatizo kwao katika dirisha hili la usajili.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here