Home World Cup Je Nahodha aliyetuhumiwa kwa madawa ya kulevya ataenda World Cup?

Je Nahodha aliyetuhumiwa kwa madawa ya kulevya ataenda World Cup?

10213
0
SHARE

*Safari Ya Urusi…*

Nahodha Wa Peru, Ruksa Kucheza Fainali Za Kombe La Dunia

Na: DANIEL S.FUTE

UONGOZI wa timu ya taifa ya Peru pamoja na watu wake wote wa taifa hilo, wamefurahishwa taarifa iliyotolewa kwamba mchezaji Paolo Guerrero ni ruksa kushiriki fainali hizo.

Taarifa hiyo imetoka hivi leo, baada ya uamuzi wa mahakama inayoshughulika na maswala ya usuluhisho wa maswala ya michezo (CAS), huko Uswisi.

Mahakama imethibitisha kwamba Guerrero, ambaye ndiye nahodha wa Peru, atakuwa huru kucheza mechi zote za fainali za Kombe la Dunia zinazo tarajia kuanza hivi karibuni huko Urusi.

Edwin Oviedo, ambaye ni Rais wa Shirikisho la Soka la Peru, alielezea kwamba “Ni furaha kubwa sana, kwa watu wote wa Peruvia”.

“Ni njia bora zaidi ya kuunganisha nchi nzima, kupitia habari hii, ambayo imewafanya watu wote wa Peru wawe na furaha.”

Guerrero alikuwa anakabiliwa na kesi ya matumizi ya madawa, ambayo si sahihi kwa wana michezo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here