Home Ligi EPL Frank Lampard ametangazwa rasmi kuwa kocha wa Derby Country.

Frank Lampard ametangazwa rasmi kuwa kocha wa Derby Country.

9312
0
SHARE

Na Melkizedeck Mbise.

Kiungo wa zamani wa Chelsea Frank Lampard ametambulishwa rasmi kuwa kocha wa Derby Country kwa mkataba wa miaka 3. Hii inakuja baada ya kocha wa timu hiyo ya ligi daraja la kwanza (Championship) Gary Rowett kuondoka na kujiunga na Stock City mnamo Mei 22, mwaka huu, baada ya timu yake kutolewa katika hatua ya mtoano (nusu fainali) na timu iliyopanda daraja Fulham. Baada ya kusaini nafasi hiyo Lampard alikaririwa akisema

“Siku zote nilikuwa nahitaji kufundisha klabu kubwa na yenye historia kama Derby Country”

*Je Lampard ni nani?*

Frank James Lampard ni mwanasoka wa Uingereza ambaye amezaliwa Tarehe 20 Juni, mwaka 1978.

*Maisha ya Soka.*

Frank Lampard alianza maisha ya soka na klabu ya soka ya West Ham mwaka 1995 mpaka 2001 ambapo alicheza mechi 148 na kufunga jumla ya magoli 24 wakati huo huo mwaka 1995/96 alipelekwa Swansea kwa mkopo akicheza mechi 9 tuu na kufunga goli 1, msimu unaofuta alirudi West Ham ambapo alocheza mpaka mwaka 2001, na baadae klabu ya Chelsea ilituma ofa kwa wagonga nyundo “The Hummer” wa London kwa dau la Euro million 11 mwaka 2001,

baada ya kutua ya kutua Chelsea ndo alianza kuwika zaidi na kuweza kutambulika katika soka barani Ulaya. Akiwa Chelsea aliweka rekodi ya kuwa kiungo aliyefunga magoli zaidi ya magoli 20 kwa kila msimu, kwa misimu 4 mfululizo kuanzia msimu wa 2005/06 mpaka 2009/10. Pia alifanikiwa kuichezea klabu ya Chelsea kwa miaka 14, Ambapo alicheza jumla ya mechi 429 na huku akifunga magoli 147 katika ligi kuu ya Uingereza.

Aidha Lampard ameichezea timu ya taifa ya Uingereza mechi 106 na kufunga magoli 29, na pia akishiriki fainali 3 za michuano ya Kombe la Dunia, wakati huo timu ya taifa ya Uingereza “Three Lions” ikifahamika kama kizazi cha dhahabu ambapo ilikua na wachezaji kama Steven Gerrad, Lampard, Rio Ferdinand, John Terry na Wayne Rooney. Ambapo licha ya kuwa na wachezaji hao hakukupata mafanikio kama kilivyotabiriwa.

*Mafanikio ya Lampard*

Frank Lampard akiwa na klabu ya Chelsea alifanikiwa kutwaa makombe 11, makombe 3 yakiwa ya ligi kuu Uingereza (Barclay premier league), makombe 4 ya FA, makombe ya ligi 2 (ambapo kwa wakati flani yalifahamika kama Carling, Capital na sasa linafahamika kama Carabao),

Europa ligi 1 na kombe 1 la ligi ya mabingwa wa Ulaya (UEFA) mwaka 2012. Ambapo mpaka Lampard anastaafu alikua amefunga jumla ya magoli 211, magoli 177 katika hayo yakiwa ya ligi kuu Uingereza.

*Maisha baada ya Chelsea*
Lampard aliondoka Chelsea mwaka 2014 na kujiunga na klabu ya New York inayoshiriki ligi kuu ya marekani maarufu kama “Major League Soccer” MLS, ambapo mwaka huo alipelekwa kwa mkopo katika klabu ya Manchester City kutokana na ubia uliopo kati ya klabu hiyo ya Marekani na Manchester City.

Hivyo alianza kuitumikia Man City mwaka 2014/15 akafanikiwa kucheza jumla ya mechi 32 na kufunga magoli 6, baadae alirudi nchini Marekani 2015/16 akicheza jumla ya mechi 29 na kufunga magoli 15, Baada ya msimu kumalizika alitangaza kusfaafu rasmi, na kujiunga na kituo cha Television cha BT Sport kama mchambuzi mpaka alivyotangazwa rasmi hii leo kuwa kocha wa Derby Country akisaini mkataba wa miaka 3.

Je ataipandisha ligi kuu Uingezera ambapo Derby wapo Championship? tusubiri kuona. Mimi namtakia maisha mema.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here