Home Kimataifa Baada ya miaka mitatu hatimaye Zinedine Zidane abwaga manyanga Real Madrid

Baada ya miaka mitatu hatimaye Zinedine Zidane abwaga manyanga Real Madrid

12500
0
SHARE

Hakuna aliyetarajia habari hii lakini ukweli ndio huu kwamba Zinedine Zidane ameamua kuachana na Real Madrid baada ya misimu mitatu mizuri ndani ya Santiago Bernabeu kama kocha.

Zilianza kama tetesi usiku wa jana kwamba huenda Zidane hatakuwa kocha mkuu wa Real Madrid katika msimu ujao na leo asubuhi kulikuwa na mkutano na raisi wa Real Madrid Florentino Perez.

“Huu ni uamuzi wangu, pengine wako watakaosema nimekosea lakini baada ya miaka mitatu naamini hili ni jambo sahihi kulifanya, klabu hii imenifanyia kila kitu na daima nitaendelea kuwa karibu na timu hii” alisema Zidane katika mkutano na waandishi wa habari.

Katika miaka mitatu ambayo Zidane amekua kocha aliiongoza Real Madrid katika michezo 149 huki wakiibuka kidedea mara 104 kwa mabao 393 huku akiwa ameshinda mechi zote za fainali wakati akiiongoza Real Madrid.

Ikumbukwe wikiendi iliyopita Zidane aliipa ubingwa wa 3 mfululizo Real Madrid katika Champions League, huku pia amewahi kuwapa La Liga 1, Spanish Super Cup 1, Uefa Super Cup 2 na Club World Cup 2.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here