Home Kitaifa Yondani katoweka Yanga

Yondani katoweka Yanga

16117
0
SHARE

Unaambiwa huko Yanga mambo ni moto mwanangu, baada ya Donald Ngoma kuachana na klabu hiyo na muda mfupi kuingia makubaliano ya kusaini mkataba na Azam, beki Kelvin Yondani haonekani Yanga.

Inaelezwa Kelvin Yondani ametoweka Yanga, simu yake haipatikani na haonekani mazoezini kwa muda sasa.

Katibu Mkuu wa Yanga  Charles Boniface Mkwasa amekiri kwamba mkataba wa Yondani unaelekea ukingoni.

“Mkataba wake haujamalizika bado upo lakini utamalizika hivi karibu na klabu imeshampa nia ya kuendelea nae kwa hiyo tusubiri muda.”

“Leo baada ya mazoezi klabu itakuwa na kikao na wachezaji wote ambao mikataba yao inaelekea ukingoni.”

“Yondani hajashiriki takribani mechi sita hivi kwa sababu tulipokea barua ya kusimamishwa kwake kucheza baada ya kutuhumiwa kumtemea mate mchezaji wa Simba.”

“Kwa hiyo alikuwa na adhabu lakini siku moja kabla ya mechi ya mwisho tukapokea barua kwamba amemaliza adhabu yake na anaruhusiwa kucheza.”

“Yeye alikuwa na matatizo ya kifamilia kwa hiyo alikuwa hajafanya mazoezi kwa muda mrefu tusingeweza kumtumia kwenye mechi iliyopita.”

Simba inahusishwa kutaka kumsaini Yondani kwa ajili ya msimu ujao.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here