Home Kimataifa #RoadToRussia, Messi ammaliza De Lima sasa amebaki Pele

#RoadToRussia, Messi ammaliza De Lima sasa amebaki Pele

11193
0
SHARE

Lione Messi amezidi kuionesha dunia kwamba yeye ni bora na atabaki kuwa bora, katika mchezo wa kirafiki hapo jana kati ya timu ya taifa ya Argentina dhidi ya Haiti Messi aligunga hattrick wakati wakiiua bao 4-0 Haiti.

Mabao 3 ya Lionel Messi yamemfanya kuivunja rekodi ya mabao mengi kwa timu za America Kusini, Messi sasa anakuwa amefikisha jumla ya mabao 64 na kumpita De Lima ambaye hadi sasa ana mabao 62.

Katika orodha hiyo sasa aliye juu ya Lionel Messi ni mshambuliaji wa zamani wa Brazil Pele ambaye hadi sasa ana mabao 77 na Messi atahitaji mabao 11 tu ili kuifikia rekodi hiyo ya Pele.

Katika orodha hiyo Romario De Souza yuko nafasi ya nne akiwa na mabao 55, Gabriel Batstuta yuko nafasi ya tano akiwa na mabao 54, Neymar Da Silva yuko nafasi ya sita na mabao 53, huku pacha wa Messi katika klabu ya Barcelona Luis Suarez akiwa na mabao 50.

Argentina mabingwa mara mbili kombe la dunia wako katika Group D la kombe la dunia wakiwa pamoja na timu za Nigeria, Crotia na Iceland na hii itakuwa michuano yao ya 16 ya kombe la dunia.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here