Home Kitaifa “Mtibwa mbona fresh tu”-Katwila

“Mtibwa mbona fresh tu”-Katwila

10115
0
SHARE
Zubery Katwila (kushoto) kocha mkuu wa Mtibwa Sugar

Kocha wa Mtibwa Sugar Zubery Katwila amesema tangu uongozi umkabidhi timu amekuwa akipata ushirikiano mzuri kutoka kwa wachezaji na uongozi wa timu hiyo.

Anaushukuru uongozi wa kiwanda kwa kumwamini kama kocha mkuu huku akiongoza benchi la ufundi kwa mara ya kwanza msimu huu baada ya kuwa kocha msaidizi kwa miimu kadhaa.

“Wachezaji naishi nao vizuri wengine kama kaka wengine kama baba kwa sababu ni wadogo wa U20, nashukuru wananielewa, wananisikiliza na kufuata kile nachotaka ukiachana na vitu vingine vidogo ambavyo mtu anaweza kukosea unamrudisha kundini tunaendelea na safari.”

“Wameniamini tangu nikiwa mchezaji, wakati nacheza Mtibwa nilikuwa captain wameona ufanisi wangu nikiwa captain wakaona uwezo ninao wa kuwa mwalimu baada ya kukaa na walimu wengine kama Maxime, Mayanga, Olaba.”

“Mayanga aliniachia katikati ya msimu nikamalizia msimu watu wengine wakaona nabahatisha lakini msimu huu nimeanza mwenyewe naelekea kumaliza na uwezo wangu wanauona.”

Shaaban Nditi ni miongoni mwa wachezaji ambao walicheza pamoja na Katwila kwenye kikosi cha Mtibwa Sugar, Katwila amesema jinsi uzoefu wa nditi unavyomsaidia kwenye timu.

“Shaaban Nditi simfundishi, namwelekeza tu kwa sababu kila kitu anacho, anauzoefu wa kucheza Mtibwa na mechi nyingine za kimataifa. Nimecheza nae kwa hiyo mimi kama mwalimu huwa namwelekeza nini nataka ananisikiliza na anafuata.”

“Hata tukiweka nidhamu ya timu wao ndio wa kwanza kufuata wachezaji wadogo na wegeni wakiona na wenyewe inakuwa rahisi kufuata inakuwa rahisi kwangu kuimarisha nidhamu kwenye timu.”

“Ushindani unapendeza, inabidi uongezeke zaidi msimu ujao kwa sababu mpira asili yake ni kushindana kwa hiyo hata mashabiki wanataka kuona ushindani na matokeo ya halali yanapatikana uwanjani.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here