Home Kitaifa Kwani kule Manungu kuna nini?

Kwani kule Manungu kuna nini?

10298
0
SHARE

Hivi unajua wachezaji wengi wanaoshindwa Simba na Yanga wanapokimbilia Mtibwa Sugar viwango vyao vinarudi?

Mtibwa ni miongoni mwa timu ambazo zinapokea wachezaji wengi kutoka Simba na Yanga baada ya kushindwa kufanya vizuri, baada ya muda wachezaji haohao wanarudi kwenye ubora wao, swali ni kwamba kuna kitu gani Mtibwa kinachorudisha viwango vya wachezaji?

Kocha wa Mtibwa Sugar Zubery Katwila kaelezea baadhi ya vitu ambavyo vimekuwa vikiwasaidia wachezaji wanaowapokea baada ya kufeli Simba na Yanga.

“Wanapata muda mzuri wa mazoezi na kubadili mazingira, anagundua alipokua alifanya makosa gani anapokuwa huku tunamsaidia kusahihisha”-Zubery Katwila.

“Wengi tuna waambia, tumekuchukua kwa sababu tunaamini una uwezo. Ukikaa na sisi ukafanya mazoezi bora ya msingi na kupumzisha mwili utarudi kwenye ubora.”

“Wanaofuata ushauri, maelekezo na mazoezi wengi wanarufisha viwango vyao wanatusaidia na wakati mwingine wanatakiwa tena na vilabu walipotoka. Kinachotakiwa ni utulivu kambini na mazoezi kwa muda.”

Wachezaji wa hivi karibuni ambao walionekana si chochote si lolote kwenye vilabu vya Simba na Yanga ni Hassan Dilunga ambaye hakuaminiwa Yanga akazunguka huku na huko amefika Mtibwa anafanya vizuri, Said Mohamed ‘Nduda’ aliwahi kusajiliwa naYanga akafeli akaenda Mtibwa sasa hivi yupo Simba.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here