Home Kimataifa John Terry Kuondoka Aston Villa

John Terry Kuondoka Aston Villa

10905
0
SHARE

Na: DANIEL S.FUTE

KLABU ya Aston Villa imetangaza kuondokewa na mchezaji wao John Terry, ambaye alijiunga na klabu hiyo msimu wa 2017/18.

Terry anaondoka klabuni hapo baada ya kumaliza mkataba wake wa mwaka mmoja, ambapo ndani yake ulikuwa na kipengele cha kuongeza mkataba kama Aston Villa ingepanda daraja na kuingia Ligi Kuu.

Aston Villa imeshindwa kupanda daraja katika mchezo wao wa mwisho wa play-off dhidi ya Fulham, ambapo walipoteza kwa bao 1-0.

Terry alihamia Villa katika uhamisho wa bure baada ya kufanya kazi huko Stamford Bridge, kwa muda wa miaka 19 na kuweza kushinda mataji matano ya Ligi kuu ya England, Ligi ya Mabingwa Ulaya na Europa League.

Mmiliki wa klabu ya Villa Tony Xia, amepokea taarifa hiyo na amesema yeye hawezi kubadilisha chochote kwa maana mkataba wa Terry tayari unajieleza.

Nyota huyo wa zamani ambay sasa ana umri wa miaka 37, alikuwa akipokea mshahara wa pauni 80,000 kwa wiki katika klabu ya Villa. Hata hivyo Terry bado hajasikika akisema anaenda wapi baada ya Villa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here