Home Kimataifa #15DaysToRussia, chukua madini haya kabla hatujakwenda Urusi

#15DaysToRussia, chukua madini haya kabla hatujakwenda Urusi

9767
0
SHARE

15, Hii ni idadi ya dribbles timilifu ambazo nyota wa Nigeria Jay Jay Okocha alipiga katika mechi ya Italia vs Nigeria mwaka 1994 ambapo Nigeria walikufa bao 2-1.

42, Hii ni idadi ya miaka ambayo mkongwe wa Cameroon Rodger Milla alikuwa nayo wakati akifunga bao dhidi ya Russia, alikuwa na miaka 42 na siku 39 na anabaki kuwa mchezaji mkongwe kufunga katika World Cup.

20, Hii ni namba ambayo timu ya taifa ya Brazil imeshiriki katika mashindano ya kombe la dunia, katika mara hizi 20 Brazil wamefanikiwa kubeba ubingwa mara 5(1958,1962,1970,1994 na 2002).

27, Mwaka 1954 timu ya taifa ya Hungary ilifunga mabao 27 katika kombe la dunia, hii bado inabaki rekodi kwa timu moja kufunga idadi kubwa ya mabao katika mashindano haya.

28, Hii ni idadi ya kadi nyekundu ambazo zilitolewa katika michuano ya kombe la dunia mwaka 2006, na hii inabaki kuwa rekodi ya kadi nyingi nyekundu katika kombe la dunia.

29, Pamoja na kuvunja rekodi ya Ronaldo De Lima hapo jana, Lionel Messi ndiye nyota anayeshikilia rekodi ya kupiga mashuti mengi langoni mwa wapinzani bila kufunga.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here