Home World Cup Uchambuzi wa kikosi cha England cha Kombe la dunia

Uchambuzi wa kikosi cha England cha Kombe la dunia

11406
0
SHARE

NIKAMA MSHALE WA WAKATI UNARUDI NYUMA KTK TIMU YA TAIFA YA UINGEREZA MAANA WAINGEREZA KIKOSI CHAO MMH TIA MAJI TIA MAJI KINA HOMA ZA VIPINDI…

Na Elizabeth Lavyule

Zikiwa zimebaki siku 16 mtifuano kuunguruma huko Urusi ktk fainali za Kombe la dunia timu nyingi zinazoshiriki mashindano haya zimeshatangaza silaha zao za maangamizi yani vimewekwa wazi vikosi vya timu zao vitavyowakilisha nchi zao ktk mashindano haya..

Kama ilivyo Kwa timu nyingine, timu ya taifa ya Uingereza maarufu kama “the three Lions” imetoa kikosi chake lakini safari hii kikiacha sintofahamu katika nafasi nyingi na kuondoa tumaini miongoni mwa wapenzi wengi Wa soka wanaoisapoti timu hiyo. Wachezaji wengi wa maeneo muhimu ni wageni hawana uzoefu katika fainali hizi kubwa mfano eneo la golini limeleta sintofahamu kwa wadau wengi wa soka.

Mlinda mlango Joe Hart aliecheza mechi nyingi za mashindano hayo makubwa ameachwa anabebwa Jack Butland wa Stock City, Jordan Pickford Wa Everton na Nick Pope Wa bunley wasio na uzoefu.

Tena hawajacheza mechi za ushindani na nchi yao tutegemee kuona makosa yatakayoigarimu timu yakijitokeza. Mfano mzuri tumewaona Liverpool wakiwa katika kiwango kizuri tu siku ya fainali ya uefa dhidi ya real Madrid Kipa mjerumani asie na uzoefu Karius anafanya uzembe unaowapa kama zawadi magoli mawili timu ya Madrid. Goli la kwanza la Benzema na la tatu la Bale kama wangekua na kipa mzoefu huenda dk 90 zingemalizika 1-1 .

Pili timu yao ina Harry Kane ni moja ya mshambuliaji bora na hatari duniani kwa sasa. Ana kila kitu inachotakiwa mshambuliaji awe nacho. Ana uweoz wa kufunga, anatoa pasi za mwisho na anachezesha timu. Tatizohakuna plani mbadala wakuchukua nafasi yake pale itakapotokea kaumia. Ifahamike amemaliza msimu Wa ligi hii akiwa na tatizo la majeraha ya mguu hivyo hayupo fiti Kwa 100%.

Wanaoweza chukua nafasi yake kama Jarmie Vardy na Marcus Rashford wanauchezaji tofauti na Kane. Wote wawili wanajua kucheza kwakukimbia nyumba ya beki sio target man (Mchezaji wa mwisho) wakati Harry Kane anafanya vyote Kwa pamoja. Mchezaji pekee anayeweza kuwa target man striker ni Danny Welbeck japo hana jicho la goli kama Kane.

Tatizo sio hilo tu, aidha kuna sintofahamu ya nani ataungana na Sterling na Kane eneo la umaliziaji. Lingard amekuwa na msimu bora katika maisha yake ya soka pale Man Utd lakini Dele Alli ndio hucheza eneo hilo. Kwa sasa ameporomoka kiwango. Ni suala la muda utatuambia kama atarudishwa eneo la kiungo kuungana na Henderson akisaidiana na Eric Dier. Mwalimu pia anaweza akamtumia kama mshambuliaji wa pili au benchi litamuhusu..

Gareth Southgate ana kazi yakuchagua katika mfumo wake wa 3-5-2 atamuamini nani acheze beki wa kulia. Kuna mambo mawili hapa. Je? Alexandre Arnold kinda wa Liverpool mwenye miaka 19 asie na uzoefu lakini ana kasi na kujiamini au atamtumia Kieran Triper beki wa Spurs ambaye ni mzuri katika umiliki wa mpira na ushambulizi au atamtumia Kyle walker tuliomzoea beki Wa man city???

Yetu macho lakini Kwa sintofahamu hizi haitakua ajabu kama England wakikwama katika hatua inayofuata kama ilivyokua fainali zilizopita kule Brazil. Michuano ile aliburuza mkia akiwa nyuma ya Croatia, Uruguay na Italy.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here