Home Kimataifa Tetesi za magazeti barani Ulaya Jumanne ya leo

Tetesi za magazeti barani Ulaya Jumanne ya leo

14419
0
SHARE

Daily Mail. Gazeti la Daily Mail limeandika habari kumhusu kocha wa Man City Pep Gurdiola, inasemekana Pep yuko karibuni kumnunua winga wa Leicester City Ryad Mahrez kwa dau la £75m.

Baada ya kumnunua Fabinho, kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amepiga hodi As Roma kwa mara nyingine na safari hii wanataka kumnunua golikipa wao Alisson Becker ili kuepuka makosa ya kizembe kama la mlinda lango wao alivyofanya dhidi ya Real Madrid.

Zaidi ya mashabiki wa soka 370,000 dunia nzima wameamua kusaini “petition” ya kuishawishi FIFA kumpiga faini mlinzi wa Real Madrid Sergio Ramos kwa kitendo cha kumuumiza Mo Salah katika fainali ya Champions League.

Pamoja na kukosa namba katika kikosi cha Manchester United lakini beki wa kulia wa klabu hiyo Luke Shaw hana mpango wa kuondoka klabuni hapo na yuko tayari kupigania nafasi katika kikosi cha kwanza.

The Sun. Gazeti la The Sun la nchini Uingereza linasema Manchester United wanaongoza katika mbio za kumnunua Gareth Bale kutoka Real Madrid, United wanatajwa kuandaa kitita cha zaidi ya £300m kumsaini nyota huyo.

United hao hao wanatajwa kuwa mbioni kumnunua Jack Grealish kutoka Aston Villa, Jose Mourinho anaaamini Grealish ana nafasi katika kikosi cha kwanza cha Manchester United.

Daily Mirror. Pep Gurdiola anaonaekana hataki utani kabisa katika kuijenga Man City, Pep yuko mbioni kumnunua Jorginho kutoka Napoli, Jorhinho amaweza kuwagharimu Manchester City kiasi cha £39m.

Liverpool wanaonekana kila sehemu katika soko la usajili, Nabir Fekir naye anatajwa kuwa kwenye rada za Jurgen Klopp. Klopp yuko tayari kumleta Fekir katika klabu ya Liverpoo kwa ada ya £60m.

Daily Telegraph. Chama cha soka nchini Uingereza FA kimeonywa kuhusu suala la kuuza uwanja wa Wembley kwa Shahid Khan. FA wameonywa kwamba kitendo cha kumuuzia Khan uwanja huo kitaleta mpasuko ndani ya chama hicho.

Klabu ya Tottenham Hotspur imehamishia majeshi Borussia Dortmund, kocha wa Dortmund Maurcio Pochettino anamhitaji Christian Pulisic katika kikosi cha Tottenham Hotspur.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here