Home Makala Kona Ya Fuku-Fuku: Ronaldo nje Bale ndani

Kona Ya Fuku-Fuku: Ronaldo nje Bale ndani

12470
0
SHARE

⚽ Sio njema hizi ⚽

RONALDO NJE, BALE NDANI KATIKA UTAMBULISHO WA JEZI MPYA ZA REAL MADRID MSIMU WA 2018/19

JUMANNE ya leo klabu ya Real Madrid, imezitambulisha jezi zake rasmi ambazo watazitumia katika msimu ujao wa 2018/19.

Jezi hizo ambazo zina dhaminiwa na kampuni ya utengenezaji wa vifaa vya michezo ‘Adidas’, imetoa jezi ya nyumbani na ugenini.

Lakini kumekuwa na maswali mengi katika utambulisho wa jezi hizo, maana mchezaji wao muhimu Cristiano Ronaldo amekosekana katika sherehe za utambulisho wa jezi hizo.

Hii imezua maswali mengi kwa mashabiki wa Real Madrid wakisema kwamba mchezaji huyo huenda asiwepo klabuni hapo mwakani.

huku na kule fukufuku ametuambia kwamba Ronaldo amegomea mkataba mpya.

Mashabiki wa Man United kama nawaona wanavyokoa macho. Mimi sipooo yangu Macho. Wadau wanauliza hivi Ronaldo akiondoka Hispania Messi si atabeba hadi tuzo za ndondo cup ya hispania?

Kingine kilicholeta maswali mengi ya utata katika utambulisho wa jezi hizo, fukfuku amesema jambo la kushangaza ni kwa mchezaji Gareth Bale ambaye inasadikika hatakuwepo katika kikosi cha msimu ujao cha Real Madrid lakini ameonekana katika wachezaji waliozitambulisha jezi hizo mpya.

Hapo majuzi ziilibuka stori mtaani kwamba Bale hataki kubakia Madrid. Rio ferdinand akamshauri bale arudi England. Kubwa zaidi ni kwamba Man United walikuwa tayari kuvunja kabati na kutoa Milioni 200.

Lakini baada ya kuibuka mchezaji bora wa UCL fainali Bale yule yule tulieambiwa anaondoka ndo kwanza anatambulisha jezi mpya ya Madrid

Hawa ni baadhi ya wachezaji waliozitambulisha jezi hizo Sergio Ramos ambaye ni nahodha wa klabu hiyo, Marcelo, Keylor Navas, Toni Kroos, Gareth Bale, Benzema na Isco.

Imeandaliwa na Daniel S.Fute

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here