Home Kimataifa Hii ndio Besiktas timu ambayo tunaweza kumuona nyota wa Ndondo anaweza jiunga...

Hii ndio Besiktas timu ambayo tunaweza kumuona nyota wa Ndondo anaweza jiunga nao

11789
0
SHARE

Hatimaye msisimko wa Ndondo Cup 2018 umezidi kuwa mkubwa, hapo jana kulikuwa na hafla ya ugawaji vifaa kwa timu pamoja na upangaji wa makundi kwa ajili ya michuano hiyo kwa mwaka.

Mengi yalizungumzwa jana lakini jambo kubwa ambalo liliibua shangwe na hamasa kwa timu za Ndondo kwa mwaka huu ni uamuzi wa moja ya wadhamini wa michuano hiyo kampuni ya Beko kuamua kumpeleka Ulaya mchezaji wa bora wa michuano hiyo kufanya majaribio katika klabu ya Besiktas.

Mwaka 1903 ndio mwaka ambao Bestikas ilianzishwa katika jiji la Instanbul nchini Uturuki huku uwanja wa Vodafone Park ukiwa uwanja wao wa nyumbani ukiwa na uwezo wa kuingiza wachezaji 41,903.

Kama hufahamu tu ni kwamba Besiktas sio klabu ya soka tu bali pia wanajishughulisha na michezo mingine ikiwemo mpira wa kikapu, mieleka, volleyball na table tennis na zote zinashiriki mashindano makubwa.

Besiktas wana rekodi nzuri sana katika ligi ya kwao nchini Uturuki ambapo wameshabeba kombe la ligi nchini kwao mara 15, kombe la Turkish National Division wamechukua mara 3 na Turkish Football Championship mara 2.

Katika michuano ya klabu bingwa Ulaya, mafanikio makubwa katika michuano hii ilikuwa msimu wa 1986/1987 ambapo Besiktas walifika hatua ya robo fainali huku mwaka 2002/2003 na 2016/2017 wakifika robo ya Europa.

Kama hujui tu Besiktas kuna nyota wakubwa duniani ambao wako Bestikas, Pepe, Ryan Babel, Alvaro Negredo na Ricardo Quaresma ni moja ya nyota maarufu katika kikosi hiki ambacho siku za karibuni tunaweza kumuona nyota mmoja kutoka Ndondo Cup akijiunga nao.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here