Home Dauda TV Yaliyojiri leo na Makundi yote ya ndondo Cup haya hapa

Yaliyojiri leo na Makundi yote ya ndondo Cup haya hapa

10219
0
SHARE

Ulikosa Uzinduzi wa Ndondo Cup? Basi nimekuletea matukio yote katika picha hapa.

Sherehe ilifana sana na Maandalizi yalikwenda vizuri.

Makundi ni kama ifuatavyo.

Nawaona wadau wa makongo hapo vijana wa Mabibo na Booooom Fc.

Kwa mtazamo wako unadhani nani atachomoka hapo?

Ilala Stand Uppp.. Naam, Washkaji zangu wa kigogo na Vijana wa Madee wa Manzese watapambana vyema na wanangu wa Kibada.

Oi oi washtue wanaaa waambie kishanuka huko

Kundi C kama hivyo unavyoliona hapo. Wazee wa kukata na shoka. Wewe kwani uko wapi hapo?

Achana na Faru John, huku ndondo sisi tuna Faru Jeuri, watamenyana vikali na wazee wa soka safi pasi 1000 magoli kibao wazee wa Burudani, njoo uone samba za kizaramo, Kampuchea na Vijana wa zamaani wa Mwana FA wa East Zoo.

Ndondo Cup mwaka huu sio mchezo. Utalikosaje kwa mfano. Huku Azam kule Clouds, Huku Beko kule DCB kisha tunaenda na Shadaka mdogo mdogo tukisindikizwa na nyumba ni choo

Wanangu wa Goms, wanangu wa Mombasa, wanangu wa KIU, akina Nyenza Goms mpoo..Watoto wa Makuburi mtakosaje yaan hili mbungi? New Life na Gorroka mtaacha vipi kusupoti chama lenu? Hebu watumie meseji wana waambieni kigoma kimelia

Asikwambie mtu mwaka huu Ndondo Cup mguu wa shingo mguu wa uso.

Pia tulipata ugenini wa watu wakubwa wakubwa si mchezo

Picha la Mwaka, Geoff lea mzee wa ung’eng’ee kibao akiwa na mzaramo. Unajiuliza hii meza ilielewana vipi hapo yaani.. Maana huyu foti foti Mbwiga nae mbwembwe kibao.

Abdi banda Nae hakukosa kuonesha upendo. Banda anakiri kuwa nae Ndondo Cup imemlea hadi kufikia kucheza Baroka ya Afrika kusini.

Mkazuzu na Boimanda nao walihakikisha kila kitu kipo sawa.

Madee yoo

Meza ilijaa watasha. sasa kama watasha wanakubali ndondo wewe unakwama vipi

wewe upo chama gani? Kama upo nje ya Dar tuambie mmejianda tujeee??

Hapo bossi akipiga ung’eng’e, hakukimbia umande….

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here