Home Kitaifa #SikuYaMwishoVPL2017/18: Ndanda, Majimaji kufa au kupona

#SikuYaMwishoVPL2017/18: Ndanda, Majimaji kufa au kupona

7159
0
SHARE

Wakati lii kuu Tanzania bara 2017/18 ikihitimishwa leo Jumatatu Mei 28, 2018 huku bingwa akiwa ameshapatikana, inasubiriwa timu moja ambayo itaungana na Njombe Mji kuiaga ligi kuu na kwenda ligi daraja la kwanza msimu ujao.

Ndanda FC na Majimaji FC ndio timu ambazo zinapambana kujikwamua zisishuke daraja. Ndanda ina pointi 26 ikiwa nafasi ya 14 wakati Majimaji yenyewe ipo nafasi ya 16 kwa pointi zake 24.

Katika mechi zao za mwisho, timu hizo zitacheza nyumani, Ndanda ikiwa mwenyeji wa Stand United uwanja wa Nangwanda Sijaona Mtwara na Majimaji ikiikaribisha Simba uwanja wa Majimaji Songea.

Kimahesabu Ndanda ina nafasi ya kubaki VPL ukilinganisha na Majimaji, Ndanda inahitaji ushindi pekee kujihakikishia kucheza VPL msimu ujao. Endapo Ndanda itashinda itafikisha pointi 29 ambazo hazitofikiwa na Majimaji hata kama itashinda mechi yake dhidi ya Simba.

Unaweza kusema Majimaji inacheza mechi ya kukamilisha ratiba kwa sababu ya nafasi yake kuwa finyu kubaki ligi kuu, inahitaji matokeo ya ushindi dhidi ya Simba lakini wakati huohuo itabidi waombe Ndanda wapoteze mechi yao.

Kama mechi hizo mbili zitamalizika kwa sare (Majimaji vs Simba na Ndanda vs Stand United) Majimaji itashuka daraja. Endapo Ndanda ikitoka sare halafu Majimaji ikashinda, timu zote zitafikisha pointi 27 kwa hiyo wastani wa magoli utaamua ambapo Majimaji ina hali mbaya katika eneo hilo ukilinganisha na Ndanda.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here