Home Kitaifa NO ujanjaujanja Ndondo Cup 2018

NO ujanjaujanja Ndondo Cup 2018

8114
0
SHARE

Michuano ya Ndondo inaendelea kuwa rasmi na ya kisasa ukilinganisha na watu walivyokuwa wanaichukulia enzi hizo.

Kuthibisha hilo ni kwamba, msimu huu fedha zote hazitatolewa wala kupokelewa mkononi, DCB Bank ndiyo bank rasmi katika kufanya miamala kwa timu zote shiriki za Ndondo Cup msimu huu.

Mwenyekiti wa kamati ya Ndondo Cup Shaffih Dauda amesema kila mwaka wanakutana na changamoto mpya. Changamoto hizo zinahusisha uendeshaji  pamoja na vilabu vyenyewe vinavyoshiriki.

“Moja wapo ya changamoto kubwa ni maswala upataji na usimamizi wa vyanzo vya pesa. Tunashukuru kwa mara ya kwanza mwaka huu tumepata mshirika wa mambo fedha DCB Bank.”

“Tunarasimisha njia zote za pesa za vilabu shiriki kwenye Ndondo Cup, ikiwemo pesa zote kutoka Ndondo Cup kwenda kwao zitapitia Bank ambayo ni DCB Bank.”

Muwakilishi wa DCB Bank amesema wapo tayari kushirikiana na Ndondo kikamilifu ili kuhakikisha vilabu shiriki vinatumia mifumo rasmi ya kifedha kwenye shughuli zao za kila siku.

DCB Bank wanasema vilabu vyote vinaweza kuwa na access ya pesa kupitia huduma ya zao kupitia simu ya mkononi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here