Home Kitaifa Ndondo Cup imetinga Ulaya mwanangu

Ndondo Cup imetinga Ulaya mwanangu

7631
0
SHARE

Ukisikia wastue wana ndio hii, hebu wastue wana wachangamkie mchongo! Ndondo Cup 2018 inapaa hadi Ulaya, ndio Ndondo inafika Ulaya kama sihara vile.

Leo Mei 28, 2018 draw ya upangaji makundi ilifanyika pale Escape One kwa ikiwa ni pamoja na kukabidhi vifaa kwa timu 32 zitakazopambana hatua ya makundi.

Baada ya makundi 8 kupangwa na kila timu kujua ipo pamoja na timu gani, ukadondoshwa mchongo utakaowafanya wachezaji wenye malengo ya kucheza Ulaya wafikie ndoto zao kupitia Ndondo.

Mchingo wenyewe upo hivi, kampuni ya Beko ni mshirika wa Ndondo Cup, Beko pia ni wadhamini wa vilabu vya Barcelona ya Hispania na Besiktas ya Uturuki, wametoa ahadi kwa mchezaji bora wa mashindano ya Ndondo Cup 2018 kwenda kufanya majaribio Ulaya.

 

“Mchezaji bora wa Ndondo Cup 2018 atakwenda Uturuki kufanya majaribio ya wiki moja kwenye klabu ya Besktas”-Jackson Picken Head of Exports Africa-Beko.

 

“Gharama zote za usafiri kwenda na kurudi Uturuki pamoja na malazi zitakuwa chini ya Beko.”

 

Besiktas JK ni mmoja ya klabu kongwe sana Nchini uturuki ikiwa na mafanikio makubwa. Besiktas ilianzishwa mwaka 1903 miaka 115 iliyopita. Besiktas wamekwisha kutwaa Ubingwa wa ligi zaidi ya mara 15.

Klabu hii kwa majina kamili inajulikana kama Beşiktaş Jimnastik Kulübü.

 

Majina ya utani ya klabu hii ni Kara Kartallar (Tai Mweusi) na jina la pili pia linaashiria sare zao, Siyah Beyazlılar (weupe na weusi)
Uwanja wao unajulikana kama Vodafone Park Beşiktaş, uliopo jijini Istanbul wenye uwezo wa kubeba watazamaji 41,903.

 

Klabu hii tokea imeanzishwa haijawahi kushuka daraja, mwaka huu wapo nafasi ya 4 kwenye msimamo wa ligi. Bwana Mehmet Şamil Şhaplı, ndiye mwanzilishi wa kwanza wa klabu hii ambapo pia yeye ni Rais wa kwanza wa klabu hii.

 

Historria ya klabu hii inaonesha kuwa baadhi ya wachezaji walifariki kwenye vita vya kwanza vya dunia kwani wengi wao waliamrishwa kwenda vitani.

 

Besiktasi pia ina akademi yao kubwa chini ya miaka 21 ambapo kama mchezaji atakuwa chini ya miaka 21 basi anaweza kupata nafasi ya kucheza katika kikosi.

 

Klabu hii ni moja ya vilabu vikubwa sana nchini humo huku ikisheheni mastaa wakubwa kama Ryan Babel pamoja na beki wa zamani wa Real Madrid, Pepe.

 

Heshima ya klabu hii ni kubwa sana kwa taifa lao. Mchezaji atayepata bahati ya kucheza klabu hii basi atakuwa amecheza moja ya vilabu vikongwe na vyenye mafanikio makubwa zaidi nchini uturuki.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here