Home Kitaifa Kocha baada ya Majimaji kushuka daraja

Kocha baada ya Majimaji kushuka daraja

9462
0
SHARE

Majimaji FC ya Songea imeungana na Njombe Mji kuiaga ligi kuu Tanzania bara, kwa maana hiyo msimu ujao watakuwa wakipambana ligj daraja la kwanza kuwabia kurejea tena VPL.

Majimaji imetoka sare ya 1-1 dhidi ya Simba kwenye mchezo wa mwisho matokeo ambayo hayakuwa na msaada wowote kwa ‘wanalizombe’ kufuatia ushindi wa Ndanda 3-1 Stand United ambao umeifanya Ndanda kubaki kwenye ligi.

Baada ya mchezo wa Majimaji dhidi ya Simba, kocha msaidizi wa Majimaji Habib Kondo amesema, mchezo haukuwa na ushindani kwa sababu Simba ilishakuwa bingwa na Majimaji ilishakata taamaa ya kubaki VPL.

“Ilikuwa haiwezekani kwetu kubaki kwenye ligi, ni sawa na Tembo kupenya kwenye tundu la sindano”-Habib Kondo.

“Safari ilikuwa na mikwaruzo mingi tangu mwanzo wa ligi, hadi tunamaliza ligi karibu wachezaji wote wa kikosi cha kwanza walishaondoka. Ukiondokewa na wachezaji 10 huwezi kufanya vizuri kwenye mashindano hususan katika ligi.”

“Matatizo ya kiuchumi ndio yakiyoigharimu timu hadi kupelekea wachezaji kuondoka.”

Kondo amesema hana mpango wa kuendelea kubaki Majimaji kwa sababu amefanya vibaya akiwa kocha wa timu hiyo.

“Kama mwalimu nimefanya vibaya, kwa hiyo sina matarajio ya kubaki Majimaji, inawezekana¬† kufanya kwangu vibaya kumetokana na matatizo ya timu lakini si kila mtu anaweza kunielewa.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here