Home Kitaifa Kama Rais anaikubali Ndondo, kwa nini tusiikubali?”-Abdi Banda

Kama Rais anaikubali Ndondo, kwa nini tusiikubali?”-Abdi Banda

8288
0
SHARE

Ndondo Cup 2018 tulimshtua mwanetu Abdi Banda beki wa Baroka FC ya South Africa na Taifa Stars kwa ajili ya kuchezesha draw ya makundi ya msimu huu.

Baada ya makundi nane (8) kujulikana, Banda amewashauri vijana kucheza na fursa iliopo mbele yao ili kutimiza ndoto zao kwenye soka.

Banda pia amesema kama Rais anaikubi Ndondo Cup kwa nini wengine wasiikubali?

“Kama Mh. Rais anaikubali Ndondo sisi kwa nini tusiikubali?”-Abdi Banda, beki wa Baroka FC ya South Afrika na Taifa Stars.

“Ndondo ya mwaka huu itakuwa kubwa kuliko ya misimu iliyopita kutoka na maandalizi yaliyofanyika, miaka uliyopita mashindano yalikuwa makubwa lakini msimu huu itakuwa zaidi.”

“Vijana watumie fursa hii kufika Banda alipo huenda wanavipaji vikubwa lakini hawakupata nafasi. Kelvin Sabato ‘Kiduku’, Idd Nado ni baadhi ya wachezaji waliotokea huku lakini tunawaona ligi kuu.”

“Mimi mwenyewe nimetoka huku kwenye Ndondo lajini leo hii nacheza nje ya nchi.”

Hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli akiwa kwenye mchezo wa kuikabidhi Simba kombe la VPL alisema, ikitokea timu ya Ndondo Cup imeshinda taji la Afrika atakwenda uwanjani kulipokea au kukabidhi kombe.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here