Home World Cup Tiketi ya Bombadia: Mambo 6 ya muhimu kuyajua

Tiketi ya Bombadia: Mambo 6 ya muhimu kuyajua

8527
0
SHARE

HOME MAKALA KOMBE LA DUNIA ZIKIWA ZIMEBAKIA SIKU 18 KUELEKEA MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA NCHINI URUSI TUANGALIE

MAMBO 6 MUHIMU.

Kombe la dunia zikiwa zimebakia siku 18 kuelekea michuano ya kombe la dunia nchini Urusi tuangalie mambo 6 muhimu.

Na Azizi Mtambo

Kichwa cha Zidane (2006).

Hi ni moja ya kumbukumbuku iliyowekwa na nguli wa mchezo huo ambaye ni kocha wa Real Madrid kwa sasa Zidane, baada ya kumpiga kichwa mchezaji wa Italy, Marco Materazzi, katika dakika ya 110, (extra time) kwa kusema alimtolea maneno machafu kuhusu Dada yake.

Rene Higuita, alivyoiponza Colombia.

Higuita, ni moja ya makipa bora kuwahi kutokea kwenye mchezo wa soka na alifahamika kwa mbwembwe zake za kuokoa mpira golini kwake pia kusaidia timu kwenye mashambulizi pale inapohitaji kushinda. Ilikuwa kombe la dunia Mwaka 1990, mechi dhidi ya Cameroon, kama kawaida yake alisogea mpaka kati kati ya uwanja na akapewa pasi na moja ya beki wake katika harakati za kutuliza aliukosa mpira huo na akauchukua mpira Rogger Milla, na kuipa Cameroon, bao la ushindi.

Mkono wa mungu

Hi ilkuwa kombe la dunia Mwaka 1986, ambapo England, walikutana na Argentina, hatua ya mtoano. mnamo dakika ya 51 Maradona, anaifungia bao Argentina, goli la mkono na kipa wa England, Peter Shilton, alipishana na mpira huo wa Maradona, na kuitwa mkono wa mungu.

Africa.

Ni moja ya Bara ambalo huwa linatoa vipaji vikubwa sana katika mchezo wa soka na kuvifanya vilabu vya Ulaya, kutegemea sana mfano George Weah, Didier Drogba, Mo Salah, Diouf, Milla, wengine wa Africa, halijwahi kupeleka timu hata moja hatua ya nusu fainali toka mashindano yaanzishwe kwa mara ya Kwanza.

Kadi nyingi katika mchezo mmoja.

Huu ni mchezo kati ya Portugal dhidi ya Holland, Mwaka 2006, nchini Ujeumani, ambao alikuwa anachezesha mwamuzi Valentino Ivanov, alimaliza mchezo huo kwa jumla ya kadi 20, njano 16 na nyekundu 4.

Pele.

Huyu ndio baba wa mchezo huu kwa zile rekodi ambazo ameziweka na ngumu kuvunjwa akiwa amefunga zaidi ya magoli 1000 katika maisha yake ya soka.

Ndiye mchezaji anayeshirika rekodi ya kuwa mchezaji wa Kwanza kucheza katika fainali hizo akiwa na umri wa miaka 17 mechi yake ya Kwanza alifunga mabao 3 na kupata ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Sweden.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here