Home Uncategorized Mh Raisi undugu wetu unamejaa wivu, unafiki na fitina

Mh Raisi undugu wetu unamejaa wivu, unafiki na fitina

8231
0
SHARE
Hivi majuzi Mh Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh John Joseph Magufuli alitembelea uwanja wetu wa taifa.

Kwenye hotuba yake alionekana kutopendezwa kabisa na aina ya mchezo wa Simba dhidi ya Kagera. nilijiuliza msawali kadha wa kadha. Hivi Mh angeona namna Yanga wanacheza si angewakataza kuvaa Unifomu za Njano na Kijani kwani zinadhalilisha chama tawala?

Mh Raisi kuna shida nyingi sana ndani ya jtawala wetu wa kimichezo. Labda nianishe kadhaa.

Kwanza hatujui thamani ya michezo ya kimataifa. Mh Raisi hivi majuzi nilimsikia msemaji mmoja kupitia kipindi cha Michezo cha Clouds akitanabaisha kuwa Zipo nchi dhaifu kariba yetu lakini zinapeleka vilabu vitatu mpaka vinne kwenye mashindano ya Afrika.


Aghalabu timu moja inapofanya vyema kutoka taifa moja kwenye mashindano haya ya kimataifa inatoa mwanya kwa taifa kuongeza idadi ya vilabu vitakavyoshiriki. Simba na Yanga vimeridhika na baghala kwa kuamini kuwa hawawezi kupata farasi.

Mh Raisi inasemekana Yanga wana matatizo ya kiuchumi. Lakini kwani ya TFF kazi yao ni nini?

Wao walipaswa kuwa mstari wa mbele kujua shida ya Yanga ni ipi na kuitatua. Kwa kuwa TFF ni baba wakimsaidia mtoto aliyeshindwa si dhambi. Yanga wapo kwenye kundi ambalo TFF kama wangekaa Sako kwa Bako na Yanga mwakani tungeongeza idadi ya vilabu vingi katika michuano ya Afrika. Mimi nina imani hili kundi la Yanga ni kachumbari tu tulihitaji chumvi kidogo.

Yanga kabla hawajaanza hii michuano ya kimataifa serikali au TFF ilipaswa ihakikishe Yanga wanasaidiwa kila kitu.
Kama kuna wachezaji walihitaji TFF ilifaa iwafanyie wepesi. Lengo sio kwa ajili ya akina Babu Akilimali Hapana! Hii ingetoa nafasi mwakani tukapeleka vilabu vitatu. Mwakani nao Simba watashiriki nao tuwabeba vivyo. Ugomvi wa vijiko wa ndugu nyumbani usipelekwe vijiweni.

Mh Raisi tumekuwa na mashabiki hayawani uwanjani.
Yaani tumekuwa na vita ya ndugu kwa ndugu utadhani tunagombania mirathi. Leo hii mashabiki wa Yanga wanawazomea Simba wakicheza na wageni na Simba vivyo hivyo. tumekuwa na chuki za batri na shahiri, hii ni balagha wala huhitaji elimu kubwa kuelewa chuki hii ya kizamani.

Labda nitoe mfano mubashara Mh Raisi.
Nafahamu unajua fika kuwa Maiti haiombwi damu.

Tunawasukuma kwa nguvu Yanga huku tunajua wana magurudumu kama mabovu. Ajali yao haitawaathiri wao tu hata majirani nao watakumbana na madhara haya. Kuna wakati Yanga wamecheza baadhi ya mechi za hapa nyumbani ilikuwa dhahiri shahiri walikuwa na wachezaji wachache. Je TFF hawakujua kama mtoto waliyemtuma gizani hakuwa na kurunzi?

Kule kwa wenzetu ulaya katika michuano ya Klabu bingwa ulaya wanaungana wote.

Ligi kuu England inapeleka vilabu vinne ulaya sawia na ligi kuu Hispania. Wanajua fika vilabu vyao visipofanya vyema basi idadi hiyo inapungua. Huwezi kusikia mshabiki wa Real Madrid anakwenda uwanja Camp Nou kuizomea Barcelona ifungwe na Chelsea. Kama haipendi hiyo klabu anabakia nyumbani tu kuliko kwenda uwanjani. Mshabiki yeyote anayejivua uzalendo na kwenda kuzomea huwa binafsi namuona kama kinyesi karibu na Meza ya chakula.


Yanga wamebingita biwi la moto kisha tunataka wafanye vyema.

Timu haina hela (Fununu), wana matatizo lukuki lakini bado ni ndugu zetu hao (bila shaka)Lakini Tusiwatenge. Watanzania tumejaa unafiki na uzwazwa hasa hasa kwenye suala la Usimba na Uyanga.


Simon Msuva alicheza Yanga. Amefanikiwa sasa anacheza soka la kulipwa huko Majuu, Cha ajabu mashabiki wa Simba leo wanamsifia kuwa mchezaji mzuri. Ni mchezaji yule yule ambaye mechi za Kimataifa tulimzomea. Vivyo hivyo kwa Mbwana Samatta.


Mechi hizi za kimataifa zina maana kubwa kwetu Mh Raisi. Kwanza zinatoa fursa wachezaji wetu kupata ajira majuu. Tunakuwa na ragbha ya kutamani soka letu lifanikiwe na lisonge mbele lakini sisi ndio wa kwanza kurudisha gurudumu letu nyuma.


Hii iwe fundisho. Mh Raisi natamani hizi mechi za Kimataifa ikiwezekana ruzuku itoke serikali watu waingie bure. Lakini ulinzi uhakikishe mnafiki yeyote atakayejali uzalendo wa usimba na uyanga peleka hata ndani. Uzalendo wa taifa letu ni wamuhimu sana.

Mh Raisi umekuwa raisi ambaye tunaweza kusema umekuwa fagio la chuma. Njoo huku kwenye soka baba. Usiishie tu uwanjani kugawa kombe. Hakikisha Simba na Yanga zinakuwa na tija kwa taifa letu.

Mh usiondoke madarakani na kutuachia soka lile lile ulilolikuta. Soka lina manufaa makubwa mno Mh. Kwa haraka haraka tuna vilabu sio chini ya 200 hapa nchini. Tuna vilabu 50 ambavyo vinacheza mashindano ya kuishindani. Tuna vilabh 20 ligi kuu. Kimahesabu tuna wachezaji 500. Nina imani kuna wachezaji 200 wanaweza wakawa wanapokea mshahara sio chini ya laki 3. Kati ya hawa wachezaji kila mmoja nyuma yake kuna watu sio chini ya watano wanamtegemea.


Yapo mashirika sio chini ya 50 yanajishughulisha na Michezo. Haya mashirika nikimaanisha vyombo vya habari n.k kila shirika lina mfanyakazi. Kilafanya kazi ana watu sio chini ya watano. Mh hujaondoa umasikini kwa watu milion 5 hapo?

Siku nikipata nafasi ya kuonana na wewe nitakweleza Mengi. Undugu wetu wa Simba na Yanga unamezwa na unafiki na wivu.

Makala hii imeandaliwa na Privaldinho. Unaweza pia kunifollow Instagram

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here