Home Kitaifa Rasmi: Ngoma ametambulishwa Azam

Rasmi: Ngoma ametambulishwa Azam

12270
0
SHARE

Baada ya Yanga kutangaza kumtema Donald Ngoma kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya muda mrefu, uongozi wa Azam FC umemtambulisha rasmi mshambuliaji huyo raia wa Zimbabwe kwa ajili ya kutumikia klabu hiyo.

Azam imeahidi kumpeleka Ngoma katika hospitali ya Vincent Pallotti Afrika Kusini kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya na matibabu.

Ngoma anatarajiwa kuitumikia Azam kuanzia msimu ujao 2018/19 ikiwa ni mpango wa Azam kuimarisha kikosi chao kwa ajili ya mapambano ya ubingwa wa VPL na mashindano mengine ikiwemo Azam Sports Federation Cup.

Azam imefunga magoli 32 katika michezo 29 ya lii kuu jambo ambalo linaonesha kuwepo udhaifu katika eneo lake la ushambuliaji baada ya kuondoka kwa nahodha wao wa zamani John Bocco, majeruhi ya Mbaraka Yusuph, pamoja na ubutu wa Bernard Arthur ambaye alitemwa pia.

Inawezekana benchi la ufundi la klabu hiyo linaamini Ngoma atasaidia kutatua tatizo hilo kwa msimu ujao.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here