Home World Cup Tiketi ya Bombadia: Mechi ya Kane Vs Hazard itapigwa hapa

Tiketi ya Bombadia: Mechi ya Kane Vs Hazard itapigwa hapa

8697
0
SHARE

Safari Ya Urusi….

Na: DANIEL S.FUTE

Inaendelea…. LEO tunafikia mwisho wa makala hii, maalumu ya viwanja 12 ambavyo vitachezewa fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018. Tulianza pamoja, acha tumalize pamoja.

Siku ya leo tunamaliza kwa kuzungumzia kiwanja cha kumi na mbili, baada ya kuvizungumzia viwanja vyote kumi na moja nyuma ambavyo ni shiriki kwa fainali hizo.

*Kaliningrad*

Kaliningrad ni Uwanja uliopo katika mji wa Kaliningrad nchini Urusi, upande wa magharibi kwenye kisiwa cha Oktyabrsky. Tofauti ya jina la uwanja huo, pia uwanja huu unajulikana kwa jina la Arena Baltika.

Unapendwa kuitwa Arena Baltika, maana huu ni uwanja mpya wa klabu ya Fc Baltika Kaliningrad. Na baada ya fainali za Kombe la Dunia uwanja huu utatumika rasmi kwa mechi za nyumbani za Fc Baltika.

Ujenzi wa kuanza kujenga uwanja wa Kaliningrad ulianza mnamo Septemba 2015, kwaajili ya fainali za Kombe la Dunia. Lakini uwanja huu ulichelewa kumalizika kwa wakati kutokana na mgogoro wa mradi uliosababishwa na shida za kifedha.

Shida hiyo ya kifedha ni baada ya kampuni ya ujenzi ambayo ilikuwa inasimamia utengenezwaji wa uwanja huo kufilisika. Lakini bado haikuwa lengo lao maana tayari mji uliwekwa kwenye ratiba ya mechi za fainali za Kombe la Dunia.

Mradi ambao ulifilisika ulikuwa na lengo la kuujenga uwanja wenye kuingiza idadi ya watu 45,000 lakini kulingana na hayo matatizo uwanja ukapunguzwa hadi kufikia kuingiza watu 35,000. Lakini pia baada ya kumalizika kwa fainali hizi utapunguzwa tena mpaka kufikia idadi ya watu 25,000 kwaajili ya matumizi ya klabu.

Rasmi uwanja huu ulifunguliwa tarehe 11 April 2018, katika mchezo wa ligi kati ya Fc Baltika na Krylia Sovetov, mchezo uliomalizika kwa Baltika kushinda bao 1-0.

Uwanja huu unatarajiwa kuchezewa mechi nne tu, katika fainali za Kombe la Dunia mwaka huu:

★16 June 2018 21:00 – Croatia vs Nigeria – Group D

★22 June 2018 20:00 – Serbia vs Switzerland – Group E

★25 June 2018 20:00 – Spain vs Morocco – Group B

★28 June 2018 20:00 – England vs Belgium – Group G

Hizo ndizo mechi ambazo zitapigwa katika uwanja wa Kaliningrad. Shukrani za dhati zikuendee ndugu mfuatiliaji wa makala hii, ambapo ulikuwa nami tangu mwanzo mwa uwanja wa Luzhniki mpaka mwisho wa Kaliningrad. ASANTE SANA.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here