Home Kitaifa Ruvu Shooting yanogesha vita ya Yanga, Azam

Ruvu Shooting yanogesha vita ya Yanga, Azam

9331
0
SHARE

Yanga wamezidi kuifanya mechi yao ya mwisho dhidi ya Azam kuwa na ushundani mkubwa wa kuwania nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi baada ya kulazimishwa sare ya 2-2 na Ruvu Shooting katika mchezo wao wa 29 wa ligi kuu.

Yanga na Azam ndiyo zitafunga msimu wa ligi, mchezo wao utachezwa Mei 28, 2018 saa 2:00 usiku uwanja wa taifa baada ya mechi nyingine zote saba za mwisho kuchezwa ambazo zitaanza saa 10:00 jioni.

Matokeo ya Yanga na Ruvu Shooting ndiyo yanaufanya mchezo wa Yanga vs Azam kuwa mtamu kwa sababu ya vita ya kuwania nafasi ya pili baada ya Simba kuwa bingwa.

Yanga imeshamaliza viporo vyake sasa ipo sawa na timu nyingine zote ikiwa imecheza mechi 29 na kukusanya pointi 52 na kuendelea kubaki katika nafasi ya pili wakati Azam yenyewe ipo nafasi ya pili kwa pointi zake 55 baada ya kucheza mechi 29.

Azam inazidiwa na Yanga kwa wastani wa magoli wa magoli sita, endapo Yanga itashinda mchezo wa mwisho dhidi ya Azam itamaliza nafasi ya pili kwa kuidizi Azam wastani wa magoli lakini timu zote mbili zitalingana pointi.

Azam inahitaji ushindi au sare ya aina yoyote ili kumaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Simba.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here