Home Kitaifa MJADALA: Kuongezeka makocha wa kigeni, Tanzania haizalishi makocha wenye viwango au...

MJADALA: Kuongezeka makocha wa kigeni, Tanzania haizalishi makocha wenye viwango au makocha wetu hawaaminiki?

6997
0
SHARE

Timu ya Alliance Academy ya mkoani Mwanza baada ya kuoanda daraja, leo Mei 24, 2018 imeingia mkataba na kocha mnyarwanda Baptista Kayiranga.

Mwaka 2004 Kayiranga alitwaa ubingwa wa ligi akiitoa Rayon aliyoichezea tangu akiwa mdogo. Aliwahi kucheza Tunisia kama mchezaji wa kulipwa akiwa winga wa kushoto.

Tofauti na Rayon Kayiranga amewahi kuzifundisha pia timu kama Kiyovu, Mukura, AS Kigali, Gicumbi na timu ya Taifa ya Rwanda ‘Amavubi.’

Mjadala umekuwa kwamba, makocha wa kigeni wanazidi kuja kuchukua nafasi Tanzania swali ni kwamba, Tanzania haizalishi makocha wenye viwango au makocha wetu hawaaminiki?

Shaffih Dauda

Klabu kama Alliance ina mlengo wa kutengeneza miundo mbinu ya soka la vijana lakini huyu kocha sijamfuatilia sana lakini namkumbuka akiwa na vilabu vya Rayon Sports, Mokula Victory ni mchezaji wa zamani wa Rayon pia.

Kwa wenzetu wa Rwanda na Burundi wanakwenda zaidi kufanya kozi za mwaka mmoja au miwili ambazo sisi tunafanya kwa wiki mbili.

Ukocha si ‘overtime job’ its a ‘permanent job’ na anaeifanya kazi hiyo kiwango chake cha elimu hakitofautiani na mtu mwingine wa taaluma tofauti kwa hiyo kiwango cha elimu na vyeti vinawabeba.

Timu kama Alliance inaonekana ina malengo ya muda mrefu, ukifuatilia ipoanzia hadi leo wanakuwa na timu ya ligi kuu ni mafanikii makubwa kwa hiyo babda wana mipango yao lazima iendane na watu wa aina fulani ndiyo maana wanalazimika kwenda kutafuta wataalam kutoka sehemu nyingine.

Kocha mtanzania ambaye tunajivunia ni Denis Kitambi ambaye alikuwa AFC Leopards lakini hivi karibuni nilikuwa namfatilia nimeambiwa amekwenda kufundisha soka Indonesia. Kocha kama huyo ukisikia kapewa timu ya taifa utasema kabebwa?

Geoff Lea

Kuna watu wanalalamika makocha wazawa hawathaminiwi, sioni sababu kwa nini watu walalamike leo hii Tanzania kuna makocha kutoka Burundi, Rwanda wanajazana hapa.

Pia sioni kwa nini makocha wa hapa hawaendi Rayon, APR kwa nini wasiende hata Djibouti au Malawi? Makocha wazawa watoke wakafundishe nje.

Neil Warnock ni kocha ambaye anaongoza kupatisha timu EPL lakini akishazipandisha katikati ya msimu anafukuzwa kwa hiyo unaona kabisa ameshindwa kudhihirisha ubora wake kwenye daraja la juu. Kwa hiyo hata makocha wetu wazawa nao waende nje kwa sababu fursa zipo, ukionesha ubora nje watu wakaona utakuja kupata kazi kubwa nyumbani.

Alex Luambano

Tunaposema watoke tujiulize pia wanakidhi vigezo? Kwa sababu kwa hizi kozi za wiki mbilimbili sidhani kama wanaweza kupata nafasi huko nje.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here