Home Kimataifa Kipi kati ya bahati au mzimu mbovu kuiamua fainali pale Kiev hii...

Kipi kati ya bahati au mzimu mbovu kuiamua fainali pale Kiev hii leo?

10594
0
SHARE

Hakuna mwenye shaka na uwezo Wa hali ya juu Wa mkufunzi Jurgen Klopp tangu akiwa na timu za Ujerumani Mainz 05 na Borussia Dortmund mpaka sasa anainoa Liverpool vijogoo wa jiji La Anfield .Klopp husifika Kwa soka safi la kasi na kuvutia na siku timu yake ikiwa katika ubora  wake, mpinzani unaadhibiwa kwa idadi kubwa ya mabao kama hutafanya juhudi za kupunguza idadi ya magoli. Katika Uefa ligue toka akiwa Borussia Dortmund Klopp amefanikiwa kucheza dhidi ya Real Madrid mechi 6 kati ya hizo ameshinda mechi tatu kapata sare mechi moja na kufungwa mbili huku akipata umaarufu Kwa soka safi wakimfunga real madrid goli 4-1 mwaka 2013 katika nusu fainali ya kwanza pale Signal Iduna Park uwanja Wa nyumbani Wa Borussia Dortmund goli zote nne zikiwekwa kambani na Mpoland Roberto Lewandowski ambaye Kwa sasa yupo katika club ya Buyern Munich.

Kwa upande Wa club ya Liverpool kitakwimu imekutana na Real Madrid mara tano ikifanikiwa kuibuka na ushindi mara tatu huku Madrid akishinda mbili tu.May 27 mwaka 1981 katika European Super Cup Liverpool alipata ushindi Wa goli moja sifuri, February 25 mwaka 2009 katika hatua ya 16 bora Liverpool alimuadhibu Madrid goli moja sifuri na March 10 mwaka 2009 ilipata ushindi mnono Wa goli 4-0 dhidi ya miamba iyo ya Santiago Bernabeu, huku Madrid Oct 22 mwaka 2014 ilipata ushindi wa 3-0 na Nov 4 mwaka 2014 Madrid akiibuka na ushindi Wa goli moja.

Lakini Kwa upande wa fainali Klop ameingia fainali mbili za usiku Wa ulaya akiwa na kumbukumbu yakupoteza fainali zote mbili mwaka 2013 alipoteza mbele ya wajerumani wenzie Buyern Munchen akifungwa goli 2-1 pia katika mashindano ya Europa ligue mwaka 2015 alipoteza kwa kufungwa goli 3-1 na Sevilla ivyo kupishana na makombe haya makubwa kabisa kwa ngazi za vilabu.

Safari hii Liverpool na Klopp kamili hawana safari rahisi kwani wanakutana na Madrid wenye nyota waliosheheni katika kikosi huku wakiwa ndio bingwa mtetezi tena akibeba kombe miaka miwili mfululizo ataweza isitisha safari ya kuwapora kombe wasibebe Kwa Mara ya tatu?Madrid ni kama wamepewa kibali na Uefa cha kuiadhibu timu yeyote wanayokutananayo fainali na sababu kubwa ya mafanikio yao Real Madrid wanajua sana kucheza na mechi zakusaka matokeo hasa katika mechi za Uefa yani hata wakicheza ovyo kufunga magoli wanajimudu mno.

Imani yangu kama Liverpool akiingia kucheza kwa kasi kama tulivyowazoea wata pata matokeo chanya na kumfanya Klopp kutoa gundu inayomtesa kutobeba ndoo kubwa ulaya lakini wakiwaacha wakina Isco wacheze wanavyotaka kama kawaida atainamisha miwani kwa maumivu hapo Kyiv kesho.

Kifo ni  kawaida kinajulikana lakini mda huez jua wala lini na nani lakini why always Klopp??tukutane kesho kujua ama historia kuwabeba majogoo Wa jiji la Liverpool ama Madrid kubeba Mara ya tatu mfululizo itafahamika kesho ktk nyasi jijini Kiev.Mohammed Salah na Cristiano Ronaldo wanatarajia kuzibeba timu zao na huenda matokeo chanya kwa klabu zao yakawafanya kua Ballon D’or Kwa mwaka ujao mana mataifa wanayotoka Ureno Kwa Ronaldo na Misri Kwa Salah hawatazamiwi kufika mbali kombe la dunia kwahiyo hii leo ndo suluhu pekee la wao kuonyesha wanastahili tuzo iyo binafsi.

By sports Dada Lizy Lyuvale

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here