Home Kimataifa #1DayToKiev, ushambuliaji wa Liverpool katika namba, hizi zinaweza kuwatisha Los Blancos hapo...

#1DayToKiev, ushambuliaji wa Liverpool katika namba, hizi zinaweza kuwatisha Los Blancos hapo kesho

9138
0
SHARE

Real Madrid vs Liverpool ni kesho, kila mtu anasubiri mchezo huu kwa hamu kubwa sana kuona je Real Madrid watabeba Champions League mara ya 3 mfululizo au Liverpool watawasimamisha? Liverpool wamekuwa na msimu mzuri sana safari hii na namba zigutazo zinaonesha namna msimu wao ulivyokuwa.

32. Hii ni idadi ya mabao ambayo mshambuliaji namba moja wa Liverpool Mohamed Salah amefunga msimu huu katika EPL, Salah amevunja rekodi ya ufungaji iliyokuwa imewekwa na Alan Shearer, Luis Suarez na Cristiano Ronaldo katika ligi hiyo.

46. Hii ni idadi ya mabao ambayo Liverpool wamefunga katika msimu huu wa Champions League, katika mabao haya 46 kuna mabao 6 ambayo waliyafunga katika hatua ya kufudhu kucheza Champions League.

20. Liverpool ni klabu ya pili katika historia ya Champions League ambayo imefunga mabao 20 katika viwanja vya ugenini msimu huu , mabao katika uwanja wa Stadio Olimpico yaliwafanya Reds kuvunja rekodi ya Real Madrid ya mwaka 2013/2014.

13. Katika michezo miwili ya Liverpool vs As Roma katika nusu fainali ya Champions League kulifungwa mabao 13. Idadi hii ya mabao pia iliifikia rekodi ya Real Madrid msimu wa 2008/2009 ambapo waliitoa Sporting Lisbon kwa mabao 12-1.

8. Hii ni idadi ya fainali za Champions League na michuano mingine ya Ulaya kwa Ujumla ambazo Liverpool wamewahi kucheza, Katika fainali hizi Liverpool walifanikiwa kubeba ubingwa wa michuano hiyo mara 5 na mara ya mwisho ilikuwa 2005 dhidi ya Ac Milan.

6. Wakati watu wakiwasifu Mo Salah, Sadio Mane na Roberto Firmnho wakipewa sifa kemkem kutokana na uwezo wao wa kufunga, Lakini 6 ni idadi ya clean sheets ambazo golikipa Loris Karius ameweka kwenye mechi 12 za Liverpool katika CL msimu huu.

2. Liverpool waliipiga Spartak Moscow mabao 7-0, na bao 7-0 vs Maribor yaliwafanya Liverpool kuwa klabu ya pili kuwahi kufunga bao 7 mara mbili katika msimu mmoja wa Champions League rekodi ambayo ilikuwa ikishikiliwa na Bayern Munich waliyoiweka mwaka 2014/2015.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here