Home Kimataifa #1DayToKiev, mfungo wa Ramadhan wazua sintofahamu kambi ya Liverpool

#1DayToKiev, mfungo wa Ramadhan wazua sintofahamu kambi ya Liverpool

11608
0
SHARE

Tuko kwenye chungu cha 9 hii leo cha mwezi mtukuf wa Ramadhan, wakati kesho tukielekea chungu cha 10 pale mjini Kiev kutakuwa na kazi kubwa ambapo Liverpool watakabiliana na Real Madrid katika fainali ya Champions League.

Mohamed Salah ni kati ya waislam ambao wanaamini sana katika mfungo wa Ramadhan, pamoja na kwamba kesho ni fainali lakini Salah katika mahojiano yake jana alithibitisha kwamba kesho ataendeleza mfungo.

Hapo juzi vyombo vya habari vya Misri vilitoa taarifa ya uhakika kwamba pamoja na ugumu wa mchezo huo lakini Mo Salah hana mpango wa kutokufunga Ramadhan, na ataacha kufunga pale mfungo utakapokwisha.

Hii leo moja kati ya watu wanaohusika na lishe kwa wachezaji wa Liverpool Ruben Pons amesema mchezaji huyo wa Misri hajafunga Ramadhan siku ya leo na hata kesho pia hatafunga ili swaumu isimuathiri katika mchezo huo.

Naye Jesus Munoz ambaye mtaalamu wa nutrionist kwa wachezaji amenukuliwa akisema kwamba kama Salah ataendeleza mfungo ni lazima imuathiri kutokana na namna wanavyofanya mazoezi kuwakabili Real Madrid hapo kesho.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here