Home Kimataifa #1DayToKiev, Cr7 anajiona bado ana miaka 23, atangaza siku yake ya kustaafu

#1DayToKiev, Cr7 anajiona bado ana miaka 23, atangaza siku yake ya kustaafu

8278
0
SHARE

Cristiano Ronaldo ameshatua Kiev kwa ajili ya fainali ya Champions League, picha aliyopost kupitia social media hapo jana ilimuonesha akiwa na Casemiro na Masero mjini Kiev wakiwa tayari wametua kuikabili Kiev.

Kama kawaida Cristiano Ronaldo alionekana amependeza sana, akipiga suti dark blue na raba nyeupe. Ronaldo achilia mbali uvaaji wake wa “kistar” lakini ana muonekano wa kijana mdogo sana pamoja na ukweli kwamba ana miaka 33.

Ronaldo amekuwa na mwili wenye muonekano uliojengeka sana na kuwa na misuli iliyopangika, siri ya muonekano huu wa CR7 anayo Luis Luvrador, Luis ni mpishi wa timu ya taifa ya Ureno na amefanya kazi hii kwa miaka 10 sasa na ikimaanisha amekuwa akimtengenezea msoc Cristiano kwa miaka 10.

Luis anasema mara nyingi Cristiano Ronaldo amekuwa akizingatia sana suala la misosi, Ronaldo amekuwa akitumia vinywaji vya kusaidia mwili kusisimka ambavyo vimekuwa vikitengenezwa na kiwango kidogo cha sukari.

Ronaldo pia amekuwa akitumia vinywaji vyenye vitamin B12 kuepuka uchovu, misosi yake Ronaldo mara nyingi imekuwa matunda fresh, anakula samaki wa aina tofauti tofauti na ndio msoc apendao na mboga za majani na nyama ya kubanika pamoja na glass ya wine.

Cristiano Ronaldo mwenyewe amekiri kwamba milo anayokula inamfanya kujisikia ana miaka 10 pungufu ya 33 aliyonayo hivi sasa, “najisikia kama niko na miaka 23 kwa sasa japo nina 33 na bado nina kama miaka 7 ya kucheza soka” alisema CR7 akimaanisha atastaafu akiwa na 41.

Hapo kesho Cristiano Ronaldo atakuwa uwanjani akijaribu kubeba ubingwa wa Champions League kwa mara ya 3 mfululizo mbele ya Liverpool, na hii itakuwa rekodi kwa Real Madrid kuwa timu ya kwanza kubeba kombe hilo mara 3 mfululizo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here