Home Ligi EPL Kocha wa Arsenal awe makini sana na mtoto wa bosi

Kocha wa Arsenal awe makini sana na mtoto wa bosi

10940
0
SHARE
Stan Kreonke amezaliwa nchini Marekani katika familia ya mjasiramali. Akiwa na miaka kumi alianza kazi ya kufagia katika kiwanda cha mbao cha baba yake.

Baadae akawa analipwa kwa kuhifadhi vitabu vya kampuni. Akiwa na miaka 16 alianza kujitegemea kwa kulipwa katika kampuni ya baba yake. Kijana huyu tayari alikuwa na damu ya kufanya biashara akiwa bado mdogo.

Damu yake ya kibiashara ilimtuma kwenda kusoma Mastazi ya Biashara aliyopata huk huko Marekani.
Stan sio kipenzi sana wa mpira wa miguu ila ni mchezaji wa zamani wa mpira wa kikapu. Kwenye soka ameingia kufanya biashara.

Kreonke mwenye umri wa miaka 70 ndiye bosi mkubwa wa Arsenal lakini chini yake kuna kiumbe anaitwa Josh Kreonke

Josh kushoto akiwa na baba yake
Josh mwenye umri wa miaka 37 ni mtoto wa Kreonke.

Huyu ndiye chachu kubwa ya Mabadiliko ya Arsenal. Alifanya Arsenal ibadilike kutoka mfumo wake wa kulea watoto na kuanza kushindana Masokoni.
Aliteuliwa Baba yake kuwa muwakilishi wake ndani ya klabu tokea 2014.

Josh ndiye sababu kubwa ya Wenger kuondoka klabuni hapo.

Mwaka huu mwezi wa Pili Josh alikwenda London. Inasemekana hakwenda kwa mema kabisa. Alifanya mabadiliko makubwa kwa kumleta Mtafiti na mkaguzi wa makubaliano ya Mikataba bwana Huss Fahmy. Pia alimwongeza mtu mwingine ambaye alishughulikia masuala ya ufanisi wa kiufundi Bwana Darren burgess.

Nakumbuka alipohojiwa alisema kwambaArsenal haiwezi kurudi katika ubora wake kama hatutakubali kufanya mabadiliko makubwa yenye tija

Josh alimleta Sven Mislintat kutoka Borussia Dortmund ambaye ni mkuu wa maskauti. Ikumbukwe huyu ndiye aliyewaleta Henrikh Mkhitaryan na Pierre Aubameyang. Pia aliyekuwa mkurugenzi wa soka la vijana wa Barcelona Raul Sanllehi aliteuliwa kuwa Meneja mahusiano wa klabu.
Hapo awali mzee Wenger alisaini mkataba mpya wa yeye kubaki klabuni hadi hapo mpaka 2019. Mkataba huu Wenger aliingia na baba yake Josh. Josh hakupendezwa kabisa na taarifa hizo kwani hapo awali alionekana kuwa karibu na Henry na alitaka kumkabidhi mikoba ya Wenger.

Josh kulia akiteta jambo na Henry

Josh alipofika London alianza uchunguzi wa hali ya juu hasa kwa Mwenendo wa Arsenal chini ya Usimamizi wa Mkurugenzi wa klabu Mzee Ivan Gazidis.

Wasemaji wa klabu walitoa taarifa kuwa Josh hakwenda kwa sababu yeyote inayomhusu Wenger ila kwa shughuli zake binafsi na za maendeleo ya klabu. Inasemekana alifanya mazungumzo na Wemger kwa Siri kwa takribani masaa mawili. Alikaa London kwa muda wa wiki tatu huku akichunguza historia ya Arsenal.

Hata hivyo alikagua miradi midogomidogo ya klabu, alikwenda viwanja vya mazoezi, na kukagua mwenendo wa akademi zote za klabu.

Ni wazi kwamba Josh alihitaji kufanya mabadiliko makubwa.

Lakini binafsi bado naona ni kama Stan na Mwanae hakuwa na maelewano mazuri hasa katika suala la Maamuzi ya mwisho ya nani arithi mikoba ya Profesa Wenger.

Josh alimhitaji zaidi Thiery Henry au Mikel Arteta.

Achilia mbali fununu za Masimillano Allegri. Tuweke mambo bayana tu wala tusiwe wanafiki.

Arsenal kwa sasa kiufanisi wapo kama Sevilla au hata Vilareal ambao ndoto yao kubwa ni kupata angalau nafasi ya 4 ili kucheza uefa.

Ni klabu ya kawaida hasa hasa kwa mwenendo wake kwa miaka ya hivi karibuni. Samahani kama nitakuwa nimekukwaza.
Kwa miaka miwili wanashindwa kabisa kurudi michuano ya UEFAna wamesuasua kupata matokeo chanya hata Yuropa.

kwa hali hii waliyo nayo Ningeshangaa sana Kumuona Wenger mpaka 2019.
Nadhani hata Josh angemsusia baba yake klabu.

Lakini tukubali baba ni Baba tu.

Baba yake amemleta Kocha ambaye sina uhakika kama ni kweli kanunuliwa kuifanya Arsenal ifikie viwango cha Real Madrid au Barcelona au hata kurudi katika zama zake.


Kwa ninavyomuona Unai Emery ni kocha wa kawaida. Sijui wewe mwenzangu.
Na pia nikimtizama sana naona ni kocha ambaye tayari amethibitisha hana viwango vya kuwanoa wachezaji wakubwa. Sijui kama tupo sawa.

Ni kocha huyu huyu aliyeshindwa kuondoa tofauti kati ya Edson Cavan, Dani Alves na Neymar Jr hadi pale Raisi wa timu alipotoa kauli yake ya mwisho.
Ni kocha huyu huyu alipoteza ubingwa kwa Monaco iliyokuwa na mshambuliaji tegemezi Falcao.


Unai sio kwamba ni mbaya sana, La Hasha! ni kocha mzuri tu. Lakini je ni wa kiwango gani. Ni wa kiwango cha kawaida. Hakuna kocha atakayetishika na ujio wa Unai pale EPL. Hatuwezi kumhofia eti kisa alitwaa Yuropa. Sasa kwani Yuropa na FA zina tofauti gani kiushindani? Mimi naona ushindani ni sawa. Ni kombe la Bonanza. Kwa mawazo yangu hasa nikipima aina ya vilabu vinayoshiriki kombe hilo utagundua ni vile vilabu vikubwa vya zamani venye viwango vibooovuu Sijui Marseille, sijui Lyon, Inter

Unai ni kocha wa Levo za Sevilla, Almeria na Valencia. Ni kocha mzuri ambaye anaweza kuhimili hali ngumu za vilabu vidogo vidogo au vya levo ya kati na akapambana vyema. Ni aibu kama leo tutamsifia Unai kuwa kocha mkubwa na wa hadhi ya Arsenal kisa tu aliwahi kutwaa vikombe vya Yuropa. Ingawa upande wa pili Arsenal nayo ni timu ya kiwango cha kati.

Kwanini Unai amepewa timu

Nipo tayari kuamini kuwa Unai hakuwa chaguo la kwanza kwa Josh. Na nipo tayari kuamini kuwa Baba yake alimtamani sana Unai muda mrefu.
Bila shaka Kwa sasa kuna makocha bora wasiozidi watano ambao ukiwachukua una uhakika wa Mafanikio katika ligi yoyote, kwa haraka haraka nao ni Pep Guardiola, Zidane na Jurgen Klopp. Hawa wengine ni wabahatishaji tu au ni makocha waliopo kwenye ligi za kawaida. Je kreonke angeweza kuwapata hawa akina Zidane?


Kreonke ni mfanyabiashara tokea awali nimesema.

Alichohitaji ni mtu atakayetimiza matakwa yake ya kibiashara. Kreonke hela zake amezipata kwa tabu. Ni tofauti kidogo na Josh ambaye yeye amekuta tayari baba ni bilionea. Josh alitaka kocha kijana ambaye atakuwa tayari kumzunguka na kujenga jina lake. Kama ilivyokuwa kwa Zidane na Guardiola. Vijana hao ni Viera, Henry na Arteta.
Hapo awali Klabu ya Rams inayoshiriki NFL nchini Marekani ilikuwa chini ya Kocha Fisher. Fisher alikuwa na matokeo mabovu sana. Baadae Josh akapigania hadi Mcay kijana wa umri wa miaka 30 akawa kocha.

Mcay alikuaa mdogo sana katika ligi lakini cha ajabu alileta mabadiliko makubwa kabla hajatwaa tuzo ya kocha bora wa mwaka. Josh alitaka kujaribu njia ile ile kwa Henry au Arteta lakini Baba yake hakuwa na wazo hilo.

Arteta aliaminika zaidi kwa kufanya kwake kazi chini ya Guardiola ni uzoefu tosha.


Arteta alihitaji hela nyingi. Kreonke tayari amekwishatumia hela nyingi. Je utamwanisha nini leo?

Ili timu ipate mafanikio ilihitaji kocha mwenye uwezo wa kununua wachezaji wakubwa na kuweza kuwamudu au ipate kocha mpya kabisa ambaye hajulikani ili kuleta chachu na hofu mpya.

Leo hii hakuna mtu anajua ubora wa Arteta hivyo lazima watu wawe na hofu.
Lakini Je Unai kuna mtu atamhofia kweli? Unai ameletwa sio kwa sababu nyingine ila tu kuzidi kuimarisha uchumi wa klabu.

Kutokana na klabu ya Arsenal kuwa katika mazingira magumu nadhani Unai sio chaguo baya lakini pia sio kocha aliyehitajika sana Arsenal kwa wakati huu..

KWANINI NASEMA AWE MAKINI

Kwanza nimeona Josh siku sio nyingi atakuwa mmiliki halali wa timu na mwenye maamuzi makubwa. Baba yake umri umeenda. Ana miaka 71. Josh anaonekana kuwa ni mtu anayetaka mafanikio. Na haogopi kutumia hela. Tokea amepewa mamlaka chini ya Baba yake amenunua wachezaji kwa gharama. Kimsingi hapa Unai atapaswa kwenda na kasi ya Josh.
Josh ataleta mastaa wakubwa. Je Unai atasuasua tena kama PSG? Josh yeye atalenga timu kwenda juu na sio kubana matumizi. Josh anataka Arsenal irudi katika zama zake.

Unai anaonekana tu kwamba ni mtu ambaye hapendi makuu. Unai ni kocha sahihi kwa baba yake. Baba anachoangalia ni timu uchumi ukue. Hivyo Unai hatohitaji sana majina makubwa klabuni. Lakini kwa Josh mhhh n tofauti kidogo.
Hata hivyo maneno yangu sio sheria huo ni mtazamo wangu tu, lolote laweza kutokea. Unai ni mwalimu mzuri anaweza kuja na mbinu mpya na akapata kile Josh anachotazamia. Makala hii Imeandaliwa na Privaldinho unaweza kunifollow Insta kwa jina hilo.

KILA LA KHERI UNAI

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here